Dec 31, 2023 08:51 UTC
  • Raila Odinga
    Raila Odinga

Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema kwamba katika mwaka mpya ataanzisha vuguvugu wa kuwahamasisha Wakenya kupinga ubadhirifu wa serikali ikiwa ni pamoja na kutoza ushuru mkubwa kuzuia fedha za elimu bila malipo na ufisadi.

Katika ujumbe wake wa mwaka mpya uliotolewa jana Jumamosi, Odinga alieleza masikitiko yake kwamba mwaka 2023 umemalizika vibaya kama ulivyoanza, Wakenya wakiendelea kutatizwa na gharama ya juu ya maisha huku kukiwa na ukimya wa serikali.

"Tutafanya kazi na watu wote wenye nia njema kurejesha matumaini na imani katika taifa letu", amesisitiza Raila Odinga na kusema: “Wakati huo ukifika, tunatarajia Wakenya wote wataweka kando tofauti zao na kushiriki katika vitendo vya kurejesha utu wa kujikimu kimaisha."

Bw Odinga amewaomba Wakenya wajitayarishe kujikomboa kutoka kwenye kile alichokitaja kuwa ukandamizaji na unyonyaji wa Serikali. Vilevile Bw Odinga ametoa onyo kali kwa Serikali kwamba muungano huo bado haujakamilisha vita dhidi ya utozaji ushuru ulioanzishwa hivi karibuni.

Kiongozi huyo wa muungano wa Azimio la Umoja ameseama anasikitishwa na opetevu wa mamilioni ya fedha zilizokusudiwa kwa mpango wa elimu bure ya msingi na sekondari, na kuziacha shule zikiwa na madeni makubwa, wanafunzi wakitaabika na walimu wakuu wakikosa fedha za uendeshaji.

Amesisitiza kuwa chama chake hakitaruhusu serikali kucheza na mustakbali wa watoto wa Kenya. 

Tags