Apr 23, 2024 03:07 UTC
  • Wagonjwa wa malaria nchini Zambia waliongezeka kwa asilimia 37 mwaka jana

Alhamisi wiki hii Zambia itaungana na nchi nyingine kuadhimisha "Siku ya Malaria Duniani" chini ya kaulimbiu ya kimataifa "Jinsia, Afya, Usawa na Haki za Binadamu."

Zambia ilishuhudia ongezeko la mwaka hadi mwaka la wagonjwa wa malaria kutoka milioni 8.1 mwaka 2022 hadi milioni 11.1 mwaka 2023. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa nchi hiyo Sylvia Masebo.

Masebo ameeleza kuwa Zambia pia imekuwa na ongezeko la asilimia 19 la vifo vlivyosababishwa na ugonjwa wa malaria kutoka vifo 1,343 mwaka 2022 hadi 1,602 mwaka jana. 

Akizungumza na waandishi wa habari wiki hii huko Lusaka, Waziri wa Afya wa Zambaia ameeleza kuwa inasikitisha zaidi kwamba asilimia 18 ya waliopatwa na malaria  walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka mitano; na asilimia moja  walikuwa wajawazito.

Masebo amesema kuwa Zambia kupitia Kituo cha Taifa cha Kupambana na Malaria imekamilisha kugawa vyandarua vyenye dawa ya kuulia mbu zaidi ya milioni 11.6 kote nchini humo.  

 

Siku ya Malaria Duniani, Aprili 25 

Waziri wa Afya wa Zambaia amesema: "Hata hivyo, lazima nisisitize kwamba kuwa na chandarua ni jambo moja, lakini muhimu zaidi ni utumiaji wake. Ili vyandarua hivi viwe na ufanisi, lazima vitumike kwa usahihi na mara zote, kila usiku na mwaka mzima.” 

Tags