Apr 23, 2024 03:08 UTC
  • Viongozi wa Afrika watilia mkazo kuzidisha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi

Viongozi wa Afrika wametoa wito wa ushirikiano zaidi wa kikanda katika kupambana na ugaidi , ikiwa ni pamoja na kuunda jeshi la kikanda. Wito huu umetolewa jana katika mkutano wa kilele wa kutafuta suluhu kwa changamoto za kiusalama zinazolikabili bara hilo mjini Abuja Nigeria.

Kuanzia nchini Mali, wanamgambo wenye misimamo ya kufurutu ada wamejiimarisha katika eneo la Sahel, wakienea kusini zaidi na kutishia mataifa ya pwani ya magharibi mwa Afrika Magharibi huku makundi mengine yanayobeba silaha yakiibua machafuko katika Pembe ya Afrika, Ziwa Chad na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Amina Mohammed Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliuambia mkutano wa kilele wa kukabiliana na ugaidi mjini Abuja kwamba: Kitovu cha ugaidi kimehama kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na kuingia katika nchi za Kiafrika  kusini mwa Jangwa la Sahara."

Bi Amina Mohammed 

"Hali ya mambo hivi sasa katika eneo la Sahel ni mbaya. Eneo hilo  linachangia karibu nusu ya vifo vyote vinavyosababishwa na hujuma za ugaidi duniani, amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.  

Katika mkutano huo wa kielle mjini Abuja, Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu aliungana na viongozi wenzake Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo na Rais wa Togo Faure Gnassingbe kuhimiza ushirikiano zaidi wa kikanda, ushirikiano katika masuala ya kiitelijinsia  na kufanya jitihada za kuunda kikosi cha jeshi.

Tags