Aug 10, 2024 06:26 UTC
  • Serikali ya Mali yamfukuza balozi wa Sweden nchini humo

Mali imemwamuru balozi wa Sweden kuondoka nchini humo ndani ya saa 72 kutokana na kauli ya "uhasama" ya waziri wa Uswidi.

Kufukuzwa kwa balozi wa Sweden nchini Mali, Kristina Kuhnel, kunakuja baada ya hatua ya serikali ya Bamako siku ya Jumatatu iliyopiita ya kutangaza kuwa inakata uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine.

Serikali ya Mali ilichuklua hatua hiyo baada ya Kiev kukiri kuhusika katika shambulio la kigaidi la hivi karibuni katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Uamuzi wa Bamako wa kukata uhusiano na Kyiv ulimfanya Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na Biashara wa Sweden, Johan Forssell, kusema Jumatano iliyopita kwamba serikali imeamua kusitisha msaada kwa Mali kutokana na uhusiano wake na Moscow.

Ni vyema kutambua kwamba, Mali na majirani zake, Niger na Burkina Faso, zimeanzisha uhusiano wa karibu na Russia badala ya Ufaransa, mkoloni wa zamani wa nchi hiyo. Nchi hizo tatu zinaituhumu Ufaransa kuwa inaingilia masuala yao ya ndani na kuendeleza ukoloni mamboleo.