Iran na Algeria zasisitiza kupanua ushirikiano wa pande mbili
(last modified Wed, 09 Apr 2025 03:03:59 GMT )
Apr 09, 2025 03:03 UTC
  • Iran na Algeria zasisitiza kupanua ushirikiano wa pande mbili

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutana na Rais wa Algeria na kubadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu zaidi ya pande mbili, kieneo na kimataifa.

Sayyid Abbas Araqchi na Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria pia wamesisitiza udharura wa kupanuliwa ushirikiano na kutekeleza makubaliano ya pande mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Rais wa Algeria wamelaani mauaji ya watu wasio na ulinzi wa Gaza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sayyid Abbas Araqchi pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Ahmed Attaf, na pande hizo mbili zimejadili na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya sasa katika uhusiano wa pande mbili na njia za kupanua ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kibiashara, kiutamaduni na kidiplomasia.

Araqchi na Attaf pia wamezungumzia mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliwasili Algiers, mji mkuu wa Algeria, jana Jumanne kwa mwaliko rasmi wa mwenzake wa Algeria.

Uhusiano kati ya Iran na Algeria umeimarika katika miaka ya hivi karibuni, na nchi hizo mbili zinajaribu kupanua zaidi uhusiano huo kwa kutilia maanani masuala yanayozikutanisha pamoja katika masuala ya kieneo na kimataifa.