Russia: Bashar Assad ni Rais halali wa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1261-russia_bashar_assad_ni_rais_halali_wa_syria
Waziri Mkuu wa Russia ametahadharisha kuwa Syria itaathiriwa na hali ya machafuko iwapo Rais Bashar Assad wa nchi hiyo atang'olewa madarakani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 15, 2016 03:08 UTC
  • Russia: Bashar Assad ni Rais halali wa Syria

Waziri Mkuu wa Russia ametahadharisha kuwa Syria itaathiriwa na hali ya machafuko iwapo Rais Bashar Assad wa nchi hiyo atang'olewa madarakani.

Akizungumzia kuhusu kuwa tayari Russia kutekeleza oparesheni za kijeshi ili kusaidia kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria na matamshi ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani juu ya uwezekano wa kuwasili nchini Syria vikosi vya nchi kavu vya nchi ajinabi iwapo mazungumzo yatafaeli, Dimitry Medvedev Waziri Mkuu wa Russia amesema kuwa, iwapo Marekani inataka kupigana vita vya muda mrefu inaweza kuanzisha vita hivyo, lakini hakuna haja ya kumtisha mtu.

Waziri Mkuu wa Russia ameongeza kuwa hakuna mtu anayetaka vita vipya na kwamba suala hilo linapaswa kuzingatiwa. Medvedev amegusia pia kuhusu mustakbali wa Bashar Assad na uungaji mkono wa Russia kwa kiongozi huyo na kueleza kuwa, hakuna dola lolote lililo na uhalali hivi sasa huko Syria ghairi ya Bashar Assad na kwamba Assad ndiye Rais mwenye madaraka.