Oparesheni ya vikosi vya Somalia dhidi ya al Shabab
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12616-oparesheni_ya_vikosi_vya_somalia_dhidi_ya_al_shabab
Askari usalama wa Somalia wamefanya oparesheni dhidi ya wanamgambo wa kundi la al Shabab na kuuwa wanamgambo kadhaa.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 04, 2016 23:45 UTC
  • Oparesheni ya vikosi vya Somalia dhidi ya al Shabab

Askari usalama wa Somalia wamefanya oparesheni dhidi ya wanamgambo wa kundi la al Shabab na kuuwa wanamgambo kadhaa.

Maafisa husika wa Somalia wameeleza kuwa shambulio lililofanywa Jumatano wiki hii na askari usalama wa Somalia dhidi ya ngome za al Shabab huko Bula-Haji lilipelekea kunaswa magari kadhaa na silaha za kundi hilo. Abdi Muhammad afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Somalia amesema kuwa jeshi la nchi huyo likishirikiana na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika kilichoko nchini humo AMISOM, limefanya oparesheni kali na kufanikiwa kulikomboa eneo la kistratejia la Grasawin lililoko umbali wa kilomita 50 mwa Hodoor kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo Francesco Madeira Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia amesema kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo kimepata mafanikio makubwa  kwa kushirikiana na jeshi la Somalia katika kurejesha amani na utulivu nchini humo tangu kikosi cha AU kilipotumwa Somalia mwaka 2007.

Wanajeshi wa kikosi cha AMISOM nchini Somalia

Kundi la wanamgambo wa al Shabab liliasisiwa huko Somalia mwaka 2006. Kundi hilo lenye misimamo ya kufurutu mipaka huko lilikuwa likiyashikilia baadhi ya maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia, ingawa mwaka jana lilipoteza udhibiti wa miji mikubwa na baadhi ya maeneo ya kistratijia.