TPLF ya Tigray yaituhumu serikali ya Ethiopia 'kuanzisha vita vya wazi'
Mamlaka katika eneo la Tigray nchini Ethiopia zimeituhumu serikali ya shirikisho kuwa kuanzisha mashambulizi ya kijeshi siku ya Jumamosi, na kufufua hofu ya kurejea vitani.
Katika taarifa, Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) imesema vikosi vya shirikisho vilitumia mizinga mikali dhidi ya maeneo yao huko Tigray Magharibi, karibu na mpaka wa pamoja na Sudan.
Baada ya miezi kadhaa ya kutumia vizuizi, mzingiro, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na vikosi vya niaba dhidi ya Tigray, TPLF imesema, serikali sasa imeanzisha "vita vya wazi."
Vyombo vya serikali ya shirikisho ya Ethiopia havijatoa maelezo yoyote kuhusu madai hayo.
Mvutano kati ya Tigray na Addis Ababa umekuwa ukizidi kuwa mbaya tangu Mkataba wa Pretoria wa 2022 uliomaliza vita vya umwagaji damu vya miaka miwili kati ya pande hizo mbili.
TPLF ilitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati, ikionya kuhusu matokeo makubwa na mabaya ikiwa vita vitapanuka.
Pia imewahimiza wakazi wa Tigray, vikosi vya usalama, vikundi vya asasi za kiraia, na taasisi za kidini kujiandaa kwa kile ilichokielezea kama mapambano ya "kubaki kwa taifa"…/