Uchaguzi wa Bunge nchini Somalia waakhirishwa tena
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i16120-uchaguzi_wa_bunge_nchini_somalia_waakhirishwa_tena
Uchaguzi wa Bunge nchini Somalia uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 24 mwezi huu hadi tarehe 10 ya mwezi ujao wa Oktoba umeakhirishwa.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Sep 26, 2016 10:43 UTC
  • Uchaguzi wa Bunge nchini Somalia waakhirishwa tena

Uchaguzi wa Bunge nchini Somalia uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 24 mwezi huu hadi tarehe 10 ya mwezi ujao wa Oktoba umeakhirishwa.

Hii ni mara ya pili kwa zoezi hilo la uchaguzi wa Bunge nchini Somalia kuakhirishwa na kuacha maswali mengi. Taarifa za awali zinasema kuwa, tofauti zilizoibuka kuhusiana na vipi wawakilishi hao wa Bunge wanapaswa kuchaguliwa ndio sababu iliyopelekea kuakhirishwa kwa uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ulipangwa kuanza mwishoni mwa wiki iliyopita na kuendelea hadi Oktoba 10 ya mwezi ujao kisha Wabunge hao kukutana tarehe 30 mwezi ujao kwa ajili ya kumchagua rais. Kutokana na tisho la usalama linaloikabili Somalia, iliamuliwa kuwa uchaguzi huo wa Bunge usiwashirikishe wanancghi wote bali wajumbe maalumu tu ambao watawachagua wawakilishi wa Bunge lijalo la nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. 

Wanamgambo wa al-Shabab wamekuwa  tishio kwa usalama wa Somalia

Takriban wajumbe 14,000 walistahili kuwachagua wawakilishi 275 wa bunge la chini na 54 wa bunge la juu; hata hivyo zoezi hilo limeakhirisha na bado haijatangazwa tarehe nyingine ya kuanza kwake.  

Tangazo la kuakhirishwa uchaguzi wa Bunge nchini Somalia linakuja siku chache tu baada ya viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kieneo ya Mashariki mwa Afrika IGAD kukutana hivi karibuni katika mkutano wao wa kihistoria mjini Mogadishu na kusisitiza juu ya kufanyika uchaguzi huo katika tarehe iliyopangwa.