Afrika Kusini yaripoti kesi ya kwanza ya Zika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1636-afrika_kusini_yaripoti_kesi_ya_kwanza_ya_zika
Afrika Kusini imethibitisha kesi ya kwanza ya kirusi cha Zika ambacho kimeingia nchini humo kupitia raia wa Colombia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 20, 2016 23:18 UTC
  • Afrika Kusini yaripoti kesi ya kwanza ya Zika

Afrika Kusini imethibitisha kesi ya kwanza ya kirusi cha Zika ambacho kimeingia nchini humo kupitia raia wa Colombia.

Kirusi hicho, ambacho kimeibua wasiwasi wa kimataifa baada ya kuenea kwa kasi kote barani Amerika, amegunduliwa nacho msafiri mmoja mjini Johannesburg, amesema Waziri wa Afya Aaron Motsoaledi.

Habari zaidi zinasema kuwa, nchi 24 duniani zimeshakumbwa na ugonjwa huo unaoenezwa na mbu. Huko nchini Brazil kumeripotiwa kesi 3,700 za watoto waliozaliwa wakiwa na ubongo mdogo, suala ambalo linazuia akili zao kukua inavyotakiwa.

Virusi vya ugonjwa huo viliibuka katika eneo kubwa la Amerika ya Latini na katika nchi za eneo la Caribbean na sasa vinaendelea kuenea katika nchi mbalimbali za dunia. Uchunguzi wa kitiba unaonesha kuwa, ugonjwa huo unazuia kukua kwa kawaida ubongo wa mtoto tumboni; na hadi hivi sasa hakuna chanjo wala dawa yoyote inayoweza kutibu au kuzuia ugonjwa wa Zika.