Feb 25, 2016 02:15 UTC
  • Kabila: Umaskini ni adui mkubwa wa Afrika

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa umaskini ndio adui mkubwa wa watu wa eneo la Maziwa Makuu ya Afrika.

Kabila amesema kuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita eneo la Maziwa Makuu ya Afrika limekumbwa na vita na migogoro na suala hilo limesababisha umaskini kati ya watu wa nchi za eneo hilo.

Rais wa Congo DR ambaye alikuwa akizungumza kwenye mkutano uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa ametoa wito wa kuundwa uchumi mmoja kati ya nchi za eneo la Maziwa Makuu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa njia pekee ya kukomesha ukatili na mapigano yaliyosababisha hasara kubwa katika eneo la Maziwa Makuu ni kuimarisha ustawi wa kiuchumi na kijamii sambamba na kutatua matatizo ya kiusalama.

Tags