Polisi watiwa mbaroni Burundi kwa kutaka kumuua msemaji wa Rais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20716-polisi_watiwa_mbaroni_burundi_kwa_kutaka_kumuua_msemaji_wa_rais
Jeshi la polisi nchini Burundi limewatia mbaroni maafisa watatu wa jeshi hilo kwa tuhuma za kushiriki katika jaribio la kutaka kumuua Willy Nyamitwe, msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 04, 2016 03:59 UTC
  • Willy Nyamitwe, msemaji wa Rais Burundi ambaye kulikuwa na njama za kumuua.
    Willy Nyamitwe, msemaji wa Rais Burundi ambaye kulikuwa na njama za kumuua.

Jeshi la polisi nchini Burundi limewatia mbaroni maafisa watatu wa jeshi hilo kwa tuhuma za kushiriki katika jaribio la kutaka kumuua Willy Nyamitwe, msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza.

Mtandao wa habari wa World Bulletin umeripoti habari hiyo na kunukuu taarifa ya jeshi la polisi la Burundi ikisema kuwa, maafisa hao watatu wametiwa mbaroni masaa machache kabla ya kufanya jaribio la kumuua msemaji huyo wa Rais wa Burundi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mlinzi mmoja wa Willy Nyamitwe aliuawa siku ya Jumatatu kwenye shambulizi ya watu wasiojulikana wenye silaha.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

 

Burundi imekumbwa na machafuko kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa yaani tangu mwezi Aprili 2015 na jitihada za kieneo na kimataifa zimeshindwa kutatua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo ndogo ya katikati mwa Afrika.

Nchi hiyo hiyo iliingia katika machafuko baada ya chama tawala cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunzinza kugombea uraia kwa mara ya tatu mfululizo. Nkurunzinza alishinda kwenye uchaguzi wa rais uliosusiwa na wapinzani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu wasiopungua 400 wameshauawa na zaidi ya laki mbili na 40,000 wamekuwa wakimbizi tangu tarehe 26 Aprili 2015 ulipoanza mgogoro wa Burundi.

Polisi wa Burundi.