Machar: Jumuiya za kimataifa zisitishe mauaji ya kimbari Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22120-machar_jumuiya_za_kimataifa_zisitishe_mauaji_ya_kimbari_sudan_kusini
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini amezitaka jumuiya za kimataifa zisaidie jutihada za kukomesha mgogoro wa kisiasa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2016 12:19 UTC
  • Machar: Jumuiya za kimataifa zisitishe mauaji ya kimbari Sudan Kusini

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini amezitaka jumuiya za kimataifa zisaidie jutihada za kukomesha mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Riek Machar amepinga pendekezo lililotolewa na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini la kufanyika mazungumzo ya kitaifa na ameuomba Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na jumuiya nyingine za kimataifa kubuni mpango mpya wa utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo na kusitisha alichokiita mauaji ya kimbari Sudan Kusini. 

Riek Machar amesema serikali ya sasa ya Sudan Kusini inafanya mauaji ya kimbari na ametoa wito wa kusitishwa mauaji hayo. 

Wakimbizi Sudan Kusini

Matamshi hayo ya makamu wa zamani wa Rais wa Sudan Kusini yametolewa siku kadhaa baada Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuonya kuhusu uwezekano wa kuibuka mauaji ya kimbari nchini humo iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa..

Machafuko ya ndani Sudan Kusini yalianza mwaka 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake, Rick Machar kwamba amehusika na jaribio la kutaka kupindua serikali yake.