Serikali ya Juba yatoa masharti ya kupelekwa askari wa UN Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i23587-serikali_ya_juba_yatoa_masharti_ya_kupelekwa_askari_wa_un_sudan_kusini
Serikali ya Sudan Kusini imetoa sharti la kupasishwa azimio jipya kwa ajili ya kupelekwa askari wa kulinda amani wa Umoja Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 16, 2017 05:21 UTC
  • Serikali ya Juba yatoa masharti ya kupelekwa askari wa UN Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imetoa sharti la kupasishwa azimio jipya kwa ajili ya kupelekwa askari wa kulinda amani wa Umoja Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Michael Makuei amesema kuwa muhula wa mwisho wa kupelekwa askari wa kimataifa wa kulinda amani katika mji wa Juba ulimalizika tarehe 15 Disemba mwaka 2016 na kwamba kupelekwa askari hao nchini humo sasa kunahitaji kupasishwa azimio jipya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tarehe 12 Agosti mwaka jana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliafiki suala la kutumwa askari wa kimataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Baadhi ya Askari wa nchi za Afrika wakiwa Juba, Sudan Kusini

Azimio la baraza hilo pia liliitaka serikali ya Juba kutayarisha mazingira ya kutumwa nchini humo askari wa nchi Kiafrika la sivyo itakabiliana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. 

Askari hao wa nchi za Afrika watakuwa na jukumu la kulinda amani na kukisaidia kikosi cha Umoja wa Mataifa kitakachokuwa na askari lfu 13.