Sudan Kusini yapinga kuweko vikosi ajinabi katika uwanja wa ndege wa Juba
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24237-sudan_kusini_yapinga_kuweko_vikosi_ajinabi_katika_uwanja_wa_ndege_wa_juba
Rais wa Sudan Kusini kwa mara nyingine tena amesema nchi yake inapinga kutumwa wanajeshi wa nchi za eneo katika uwanja wa kimataifa wa Juba mji mkuu wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 25, 2017 11:38 UTC
  • Sudan Kusini yapinga kuweko vikosi ajinabi katika uwanja wa ndege wa Juba

Rais wa Sudan Kusini kwa mara nyingine tena amesema nchi yake inapinga kutumwa wanajeshi wa nchi za eneo katika uwanja wa kimataifa wa Juba mji mkuu wa nchi hiyo.

Rais Salva Kiir leo ametamka bayana kuwa nchi yake inapinga kutumwa vikosi ajinabi vya kieneo katika uwanja wa ndege za kimataifa wa Juba.

Juba International Airport 

Rais wa Sudan Kusini amesema kuwa haafiki suala hilo la kutaka kudhibitiwa uwanja huo wa ndege wa kimataifa na vikosi ajinabi. Olf Skog Balozi wa Sweden katika Umoja wa Mataifa ambaye mwezi huu wa Januari amechukua uwenyikiti wa Baraza la Usalama la umoja huo, amewasilisha tena takwa la Baraza la Usalama la kutumwa haraka iwezekanavyo wanajeshi wa nchi za eneo huko Sudan Kusini. Kikosi hicho kitaundwa na wanajeshi elfu nne wa nchi za Kiafrika na Umoja wa Mataifa pia ndio unafungamana na kikosi hicho.