UN hali ya jela nchini Tunisia inatia wasiwasi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24691-un_hali_ya_jela_nchini_tunisia_inatia_wasiwasi
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hali ya jela za Tunisia inatia wasiwasi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 04, 2017 12:52 UTC
  •   UN hali ya jela nchini Tunisia inatia wasiwasi

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hali ya jela za Tunisia inatia wasiwasi.

Ripota wa haki za binadamu na kupambana na ugaidi wa Umoja wa Mataifa aliyeko nchini Tunisia, Ben Emmerson amesema hali ya jela ya Mernaqia nchini Tunisia inapingana na vigezo vya kimataifa na kwamba hali hiyo inakiuka haki za mahabusu hususan wale wanaokabiliwa na tuhuma za ugaidi.

Ben Emerson ambaye anatazamiwa kuwasilisha ripoti kamili katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hapo mwakani, amewataka maafisa wa serikali ya Tunisia kuwa macho kuhusu mateso na mienendo mibaya wanayokabiliana nayo mahabusu na kutazama upya sheria ya ugaidi ya mwaka 2015 ambayo inaruhusu kurefushwa kipindi cha kushikiliwa mahabusi kwa siku 15 zaidi bila ya kujulishwa tuhuma zao.

UN: Hali katika jela za Tunia inatia wasiwasi

Safari ya ripota wa haki za binadamu na kupambana na ugaidi wa Umoja wa Mataifa nchini Tunisia, Ben Emmerson ndiyo ya kwanza kufanywa na afisa wa ngazi za juu wa umoja huo nchini humo tangu mwaka 2011.