Burundi yaitaka serikali ya Tanzania iwatie mbaroni wapinzani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25334-burundi_yaitaka_serikali_ya_tanzania_iwatie_mbaroni_wapinzani
Serikali ya Burundi imeitaka Tanzania iwatie mbaroni wapinzani hao ambao wanashiriki kikao cha mazungumzo ya amani huko kaskazini mwa Tanzania huku wakiwa wanatafutwa na mahakama ya nchi hiyo kwa kuhusika na mapinduzi yaliyofeli.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 18, 2017 23:12 UTC
  • Burundi yaitaka serikali ya Tanzania iwatie mbaroni wapinzani

Serikali ya Burundi imeitaka Tanzania iwatie mbaroni wapinzani hao ambao wanashiriki kikao cha mazungumzo ya amani huko kaskazini mwa Tanzania huku wakiwa wanatafutwa na mahakama ya nchi hiyo kwa kuhusika na mapinduzi yaliyofeli.

Bernard Ntahiraja, Naibu wa Alain-Aimé Nyamitwe, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Burundi amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa waliohusika na mapinduzi hayo ya kijeshi, wameshiriki katika mazungumzo ya amani ya mjini Arusha Tanzania, ambayo yaliitishwa kwa lengo la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Rais Nkurunziza wa Burundi

Hii ni katika hali ambayo Jumatano iliyopita, Philippe Nzobonariba, Msemaji wa serikali ya Burundi alitangaza kuwa serikali ya Bujumbura haitoshiriki mazungumzo hayo kutokana na kile alichokisema kuwa ni ushiriki wa wapinzani walioshiriki katika jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Pierre Nkurunziza. Mgogoro wa Burundi uliibuka mwezi Aprila mwaka 2015 baada ya Rais Nkurunziza kutangaza azma yake ya kugombea katika uchaguzi wa rais uliopita kwa muhula wa tatu, hatua iliyotajwa na wapinzani kuwa ni kinyume na katiba.

Juhudi za upatanishi za Benjamin Mkapa

Kwa mujibu wa Philippe Nzobonariba, mazungumzo hayo ya mjini Arusha na yaliyosimamiwa na Benjamin Mkapa rais wa zamani wa Tanzania, yatatatiza juhudi za kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.