Mar 06, 2017 04:00 UTC
  • Waasi Sudan wawaachia huru wafungwa 127

Waasi wanaopigana dhidi ya serikali katika maeneo ya kusini mwa Sudan wamewaachia huru mateka 127 huku jeshi la nchi hiyo likikaribisha hatua hiyo.

Jeshi la Sudan lilisema jana Jumapili kuwa wafungwa hao walioachiwa huru ni pamoja na wanajeshi 109 na raia 18 ambao walitekwa nyara na waasi wa harakati ya SPLM-N katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini. Msemaji wa jeshi la Sudan Brigedia Ahmed Khalifa al Shami amepongeza kuachiwa huru mateka hao na kukitaja kitendo hicho kuwa ni hatua kubwa kuelekea kufikiwa amani ya kudumu katika majimbo ya kusini mwa Sudan yaliyoathiriwa na hali ya mchafukoge. Mapigano yalizuka katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini mwaka 2011 baada ya waasi kusema kuwa wamechoshwa na sera za ukandamizaji za serikali ya Khartoum katika majimbo hayo mawili.

Mateka walioachiwa huru na waasi wa Sudan 

 

 

 

Tags