Jeshi la Tunisia lafyatua risasi angani kuwatawanya waandamanaji
Jeshi la Tunisia limefyatua risasi angani kuwatawanay waandamanaji waliokuwa wanajribu kuzuia uchimbaji gesi katika mkoa wa Tatatouine kusini mwa nchi hiyo.
Wananchi waliokuwa na hasira waliandamana Jumamosi na moja ya madai yao makuu ni kupata ajira katika vituo viwili vya kuchimba gesi aktika eneo hilo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo wiki iliyopita, Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia aliamuru jeshi la nchi hiyo kulinda vituo vya kuchimba gesi na mafua baada ya waandamanaji kujaribu kuvuruga uzalishaji katika vituo hivyo vilivyo kusini mwa nchi.
Hii ni mara ya kwanza wanajeshi nchini Tunisia kutumiwa kwa ajili ya kulinda vituo hivyo vyenye umuhimu mkubwa kwa uchumi wa nchi hiyo. Hatua ya migomo na maandamano ya wafanyakazi katika vituo hivyo imepelekea Tunisia kupoteza mabilioni ya dola katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa wiki kadhaa sasa watu karibu 1,000 mkoani Tatouine ambapo mashirika ya ENI la Italia na OMV la Austria yanachimba mafuta, wamekuwa wakiandamana kutaka kazi na pia wanadai kupewa sehemu ya pato la utajrii wa mali asili katika eneo hilo. Maandamano pia yameripotiwa katika mkoa wa Kebili kusini mwa nchi.
Hivi sasa, miaka sita baada ya mapinduzi ya wananchi kuleta demokrasia nchini humo, Tunisia inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira hasa miongoni mwa vijana wa kusini mwa nchi hiyo ambao wanahisi kutengwa.