Jul 24, 2017 07:14 UTC
  • Makumi wauawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila magharibi mwa Sudan

Watu 28 wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan.

Maafisa katika jimbo hilo wameeleza kuwa watu kumi wameuawa katika mapigano yaliyojiri kati ya watu wa makabila mawili hasimu ya Kiarabu ya al Ma'aliya na al Raziqati umbali wa kilomita arubaini kusini mashariki mwa mji wa al Dinh huko Darfur. 

Kabla ya kujiri mapigano hayo, mwezi Aprili uliopita pia watu 9 waliuawa katika mapigano kama hayo kati ya makabila hayo mawili hasimu ya Kiarabu huko Darfur. Mapigano mapya ya kikabila yanajiri jimboni Darfur huku Umoja wa Mataifa ukijiandaa kupunguza idadi ya askari wake wa kulinda amani katika eneo hilo.  

Makundi yanayobeba silaha jimboni Darfur  

Mapigano yalianza katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan tangu mwaka 2003 huku makabila yanayobeba silaha yakiituhumu serikali kwa kuwabagua watu wa eneo hilo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa mzozo wa Darfur umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki tatu na kuwafanya wakimbizi raia wengine milioni mbili na laki tano. 

Raia wa jimbo la Darfur waliolazimika kuwa wakimbizi kufuatia mapigano  

 

Tags