Aug 24, 2017 13:46 UTC
  • Jeshi la Niger lashambulia maficho ya Boko Haram; magaidi 40 wauawa

Jeshi la Niger limeshambulia moja ya maficho ya kundi la kigaidi la Boko Haram kusini mashariki mwa nchi hiyo katika fremu ya oparesheni ya kuwaangamiza magaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Maafisa wa kijeshi wa Niger leo wamearifu kuwa magaidi 40 wa kundi la Boko Haram wameangamizwa katika shambulio hilo. Wameongeza kuwa vikosi vya nchi hiyo vimekabiliana na  magaidi wa kundi la Boko Haram katika oparesheni ya doria iliyotekelezwa na jeshi la Niger katika eneo la Diffa nchini humo. Jeshi la Niger lilianza kutekeleza oparesheni ya kuwasaka magaidi wa Boko Haram katika eneo la Diffa tangu wiki iliyopita.

Wanajeshi wa Niger wakiwa katika doria katika eneo la Diffa nchini humo

Mwanajeshi mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika oparesheni hiyo. Eneo la Diffa huko kusini mashariki mwa Niger linakabiliwa na ukosefu wa amani kufuatia kuwepo maficho ya magaidi wa kundi la Boko Haram. Kundi hilo limezidisha mashambulizi yake ili kuzusha hofu katika kambi za wakimbizi zilizopo katika eneo la Diffa. 

Tags