Oct 23, 2017 03:18 UTC
  • OIC yalaani mauaji ya Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na taasisi ya al Azhar nchini Misri zimelaani mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali mauaji yaliyofanywa dhidi ya Waislamu katika maeneo ya kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na imetoa wito wa kupelekwa haraka misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa mashambulizi hayo ya kinyama. 

Wakati huo huo taasisi ya Azhar nchini Misri imelaani pia mauaji ya Waislamu wasio na hatia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yanayofanywa na kundi la kigaidi la Anti Balaka na imetoa wito wa kusitishwa mara moja mashambulizi ya yanayofanyika kwa chuki za kidini na kikabila. Al Azhar pia imetaka kuchukuliwe hatua za kukabiliana na mashambulizi ya kundi hilo. 

Magaidi wa Anti Balaka, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Waasi wa kikristo wa kundi la Anti Balaka tarehe 19 mwezi huu wa Oktoba walifanya mauaji ya kutisha na ya kinyama ya zaidi ya Waislamu 150 na kujeruhi makumi ya wengine.

Tarehe 13 mwezi huu wa Oktoba pia magaidi hao walishambulia msikiti katika mji wa Kimbi, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuua Waislamu 25 akiwemo imamu wa jamaa wa msikiti huo na msaidizi wake.   

Tags