Rais wa Misri alifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3664-rais_wa_misri_alifanyia_mabadiliko_baraza_lake_la_mawaziri
Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri na kuwateua mawaziri kumi wapya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 23, 2016 21:25 UTC
  • Rais wa Misri alifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri na kuwateua mawaziri kumi wapya.

Mabadiliko hayo katika Baraza la Mawaziri la Misri yaliyofanywa jana na Rais Abdel Fattah al Sisi yameingiza sura mpya kumi serikalini huku kukiwa hakujatolewa taarifa yoyote rasmi kuhusu sababu iliyompelekea Rais wa Misri kulifanyia marekebisho baraza hilo la mawaziri. Hata hivyo mabadiliko muhimu yametajwa kuzigusa Wizara za Fedha, Uwekezaji na Rasilimali za Maji.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hatua ya Rais wa Misri ya kuwateua shakhsia kutoka sekta binafsi kuongoza Wizara za Fedha na Uwekezaji inaakisi imani hii kwamba watu wenye uzoefu kutoka sekta binafsi wana uwezo katika kuhuisha uchumi unaolegalega wa nchi hiyo. Wengine wanasema kuwa Waziri wa Maji amebailishwa wadhifa wake kufuatia kuzorota kwa mchakato wa mazungumzo kati ya Misri na Ethiopia, kuhusu ujenzi wa bwawa kubwa katika Mto Nile unaofanywa na Ethiopia, ujenzi ambao utapunguza mgawo wa Misri wa maji ya mto huo.