Jeshi la Ethiopia laua raia 9, ladai lilidhani ni waasi
(last modified Tue, 13 Mar 2018 02:44:21 GMT )
Mar 13, 2018 02:44 UTC
  • Jeshi la Ethiopia laua raia 9, ladai lilidhani ni waasi

Jeshi la Ethiopia limetangaza kuua raia tisa na kuwajeruhi wengine 12 na kudai kuwa lilidhani ni waasi walio katika eneo linalopakana na Kenya.

Wanajeshi hao ambao walikiwa wametumwa katika eneo la Moyale katika jimbo la Oromiya kuwasaka waaasi wa  Harakati ya Ukombozi wa Oromo. Shirika Rasmi la Habari la Ethiopia limesema jeshi limekiri kuwaua raia tisa na kuwajeruhi wengine na kusema raia hao wameuawa kimakosa kutokana na taarifa zisizo sahihi za upelelezi. Duru zinadokeza wanajeshi husika wamesimamishwa kazi na wanachunguzwa huku ujumbe wa ngazi za juu wa kijeshi ukitumwa kuchunguza tukio hilo. Raia wengi katika upande wa Ethiopia wamekimbilia nchi jirani ya Kenya kwa hofu kuwa wanajeshi wanaweza kuendeleza mauaji hayo yaliyojiri mwezi Februari.

Harakati ya Ukombozi wa Oromo ni kundi la waasi wanaotaka eneo la Oromiya lijitenga na Ethiopia na serikali inaitaja harakati hiyo kuwa ni kundi la kigaidi.

Wanajeshi wa Ethiopia

Hayo yanajiri wakati ambao mwezi uliopita, serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya hatari nchini humo siku moja baada ya kujiuzulu Hailemariam Desalegn Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Viongozi wa Ethiopia wamesema kuwa hali ya hatari imetangazwa nchini humo kufuatia pendekezo la serikali kwa lengo la kulinda katiba na kuzuia kuzuka machafuko nchini humo.