Waziri wa zamani wa ulinzi wa Somalia achaguliwa kuwa Spika wa Bunge
May 01, 2018 04:15 UTC
Wabunge wa Somalia jana walimchagua Mohamed Mursal Abdirahman, waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo kuwa Spika mpya wa Bunge.
Katika kura iliyopigwa jana Jumatatu, waziri huyo wa zamani wa ulinzi wa Somalia alipata kura 147 za wabunge na kumshinda mpinzani wake Ibrahim Isak Yarow aliyepata kura 118.
Mohamed Mursal Abdirahman alijiuzulu nafasi ya waziri wa ulinzi wiki iliyopita ili kujiandalia mazingira ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge.
Spika wa zamani wa bunge la Somalia, Mohamed Osman Jawari alilazimika kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Aprili kutokana na mashinikizo ya Serikali.
Somalia inahesabiwa kuwa moja ya nchi maskini zaidi na yenye usalama mdogo zaidi ulimwenguni.
Tags