Kushtadi ghasia Afrika Kusini kutokana na huduma mbovu na umaskini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48872-kushtadi_ghasia_afrika_kusini_kutokana_na_huduma_mbovu_na_umaskini
Ghasia na machafuko yanayoendelea kuikumba Afrika Kusini kutokana na wananchi kutoridhishwa na huduma mbovu na umaskini zimeongezeka pakubwa katika mwaka huu wa 2018. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa jana Jumatano.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Oct 18, 2018 00:42 UTC
  • Kushtadi ghasia Afrika Kusini kutokana na huduma mbovu na umaskini

Ghasia na machafuko yanayoendelea kuikumba Afrika Kusini kutokana na wananchi kutoridhishwa na huduma mbovu na umaskini zimeongezeka pakubwa katika mwaka huu wa 2018. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa jana Jumatano.

Weledi wa mambo wanasema kuwa ghasia hizo ni ishara kwamba chama tawala cha Kongresi ya Taifa hakipasi kuzipuuza kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahidi kuboresha utendaji wa serikali na kufufua uchumi wa nchi hiyo hata hivyo kutoridhishwa pakubwa wananchi kunaashiria changamoto zinazokikabili chama cha ANC katika kipindi hiki ambacho kinajaribu kufufua uchumi wa nchi hiyo iliyokuwa na uchumi mzuri wa viwanda. 

Maandamano nchini Afrika Kusini yameshuhudia kuenea katika maeneo yanayodhibitiwa na pande zote mbili yaani chama tawala ANC na mrengo wa upinzani huku ghasia nyingi zikiripotiwa kutokea katika jimbo la Cape ya mashariki ambayo ni ngome kuu ya chama tawala ANC ambacho kimekuwa katika hatamu za uongozi nchini Afrika Kusini tangu kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo mwaka 1994.

.