Kiongozi wa zamani Madagascar aongoza matokeo ya awali uchaguzi wa rais
(last modified Thu, 08 Nov 2018 08:26:38 GMT )
Nov 08, 2018 08:26 UTC
  • Kiongozi wa zamani Madagascar aongoza matokeo ya awali uchaguzi wa rais

Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais limekuwa likiendelea mapema leo huko Madagascar huku kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Andry Rajoelina akiongoza matokeo ya awali kwa mujibu wa kura zilizohesabiwa katika vituo vichache nchini humo.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa leo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Madagascar (INEC) kwa mujibu wa kura kutoka vituo vya uchaguzi visivyopungua mia moja kati ya zaidi ya elfu 24 yanaonyesha Rajoelina anaongoza kwa kura 44.4 akiwapita mahasimu wake wawili wakuu. Mahasimu hao ni Hery Rajaonarimampianina na Marc Ravalomanana. Uchaguzi wa rais wa mwaka huu katika kisiwa cha Madagascar unawakutanisha pamoja wagombea 36.

Mahasimu wakuu wa kiti cha urais Madagascar

Wapiga kura nchini humo wamesema kuwa wanataraji watampata Rais ambaye ataweza kuzipatia ufumbuzi changamo nyingi zinazoikabili nchi hiyo maskini likiwemo suala la ukosefu wa ajira na ufisadi.

Akizungumza na wafuasi wake jana katika makao makuu ya kampeni huko Antananarivo, Andry Rajoelina amewaahidi kuibuka na ushindi na amewataka wawe watulivu.