Jan 11, 2019 01:13 UTC
  • Jinai za magaidi wa Boko Haram zimeshika kasi nchini Nigeria

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, magaidi wa Boko Haram wanawalazimisha wananchi wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kuzihama nyumba zao.

Katika taarifa yake jeshi hilo limesema kuwa, kwa mujibu wa taarifa za kuaminika lilizo nazo, magaidi wa Boko Haram wamewalazimisha wakazi wa vijiji vya karibu na Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno, wazihame nyumba zao.

Taarifa hiyo ya jeshi la Nigeria imeongeza kuwa, magaidi wa Boko Haram wanatoa vitisho vikali kwa watu wa kawaida na inawatisha kuwa wazihame nyumba zao kabla hawajauawa.

Wakazi wa eneo la Baga, kaskazini mashariki mwa Nigeria wakiangalia uharibifu uliofanywa na magaidi wa Boko Haram

 

Siku ya Jumatano Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa, zaidi ya watu 30,000 wamezihama nyumba zao katika maeneo ya Baga na Monguno karibu na Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno wamezikimbia nyumba zao.

Edward Kallon, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa alitangazasiku ya Jumatano kwamba, katika wiki za hivi karibuni zaidi ya wakimbizi elfu 30 wengi wao wakitokea eneo la Baga wamewasili katika mji wa Maiduguri huko kaskazini mashariki mwa Nigeria kukwepa mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na  afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ilisema kuwa, mapigano makali yaliyotokea baina ya jeshi la Nigeria na magaidi wa Boko Haram karibu na Ziwa Chad mwishoni mwa mwezi uliopita yamewalazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu. 

Tags