Mahakama ya Misri yafuta hukumu ya kifo dhidi ya wapinzani 149
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i517-mahakama_ya_misri_yafuta_hukumu_ya_kifo_dhidi_ya_wapinzani_149
Mahakama ya Rufaa nchini Misri imefuta hukumu ya kifo iliyokuwa imetolewa hapo awali dhidi ya wapinzani 149 wa serikali nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2016 10:51 UTC
  • Mahakama ya Misri yafuta hukumu ya kifo dhidi ya wapinzani 149

Mahakama ya Rufaa nchini Misri imefuta hukumu ya kifo iliyokuwa imetolewa hapo awali dhidi ya wapinzani 149 wa serikali nchini humo.

Mahakama ya Rufaa ya Misri imefuta hukumu ya kunyongwa dhidi ya wanaharakati 149 wa Ikhwanul Muslimin iliyokuwa umetolewa baada ya kushambuliwa kituo kimoja cha polisi na kuuawa askari kadhaa wa usalama wa nchi hiyo.

Mahakama hiyo ya Misri imeagiza kuhukumiwa upya watuhumiwa hao wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.

Askari usalama 13 wa Misri waliuawa mwezi Agosti mwaka juzi katika shambulio lililofanywa katika kituo kimoja cha polisi karibu na Cairo mji mkuu wa nchi hiyo.

Vikosi vya usalama vya Misri mwezi Agosti mwaka 2014 waliwauwa kwa kuwapiga risasi mamia ya wafuasi wa Ikhwanul Muslimini waliokuwa wakiandamana.