Aug 15, 2019 13:19 UTC
  • Marais wa Tanzania na Afrika Kusini wapigia debe fursa za uwekezaji

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani amewakaribisha wafanyabiashara wa Afrika Kusini kwenda kuwekeza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za afya, hoteli, utalii wa fukwe na uchakataji wa madini

Rais Magufuli amesema hay oleo ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo yake na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye aliwasili nchini Tanzania hapo jana kwa ziara ya siku mbili na baadaye atashiriki katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za Juumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais Magufuli amesema kuwa, Tanzania imetenga kila mwaka zaidi ya sh270 bilioni kwa ajili ya kununua dawa na vifaa vya tiba na asilimia 98 ya fedha hizo zinakwenda kuununua nje ya nchi; hivyo amewakaribisha wafanyabiashara wa Afrika Kusini kwenda kuwekeza Tanzania katika sekta hiyo kwani ni fursa kubwa.

Aidha Rais Magufuli amemhakikishia Rais Ramaphosa kwamba, Tanzania itanunua vifaa ambavyo vinatengenezwa Afrika Kusini badala ya kwenda kununua nchi za mbali.

Kwa upande wakke Rais Cyril Ramaphosa amewakaribisha wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini Afrikka Kusini na kueleza kwamba, ni muhimu kwa nchi hizo kutumia fursa zinazojitokeza kwa manufaa ya wananchi wao.

Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 17 mwezi huu wa Agosti jijini Dar es Salaam ikiwa imepita miaka 16 tangu mkutano kama huo ufanyike kwa mara ya mwisho katika katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Tags