May 19, 2021 06:28 UTC
  • UN yaiomba Tanzania iwape hifadhi raia wa Msumbiji wa Cabo Delgado wanaokimbia mapigano

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UBHCR limesema lina wasiwasi mkubwa na taarifa zinazoendelea za watu wanaokimbia jimboni Cabo Delgado nchini Msumbiji kurudishwa kwa nguvu baada ya kuvuka mpaka kuelekea nchi jirani ya Tanzania.

Akizungumza na wanahabari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa UNHCR Boris Cheshirkov amesema shirika hilo la UN na wadau wake wamepokea ripoti za kutia wasiwasi pamoja na ushuhuda wa moja kwa moja kwamba maelfu ya watu kadhaa wa Msumbiji wamerudishwa nyuma kutoka Tanzania kuelekea kaskazini mwa Msumbiji tangu mwaka jana hii ikijumuisha ripoti kuhusu raia zaidi ya 1,500 wa Msumbiji waliorudishwa mwezi ulioipita.

 Mwezi uliopita wa Aprili na katika mpaka wa Negomano kaskazini mwa Msumbiji, UNHCR na wadau wake waligundua kuwa watu wengi wa Msumbiji walioko huko walitarajia kupata kimbilio nchini Tanzania baada ya kukimbia mashambulio mabaya wa makundi ya wanamgambo wanaopinga serikali katika eneo la Palma mnamo mwezi Machi. Watu hao waliiambia UNHCR kuwa walisafiri kwa siku kadhaa katika mto Ruvuma, wakivuka kwa mashua kufika Tanzania, ambako walirudishwa na mamlaka za nchi hiyo jirani. Wengi walikuwa wanawake na watoto wadogo. 

Raia wa Msumbiji waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na machafuko katika eneo la Cabo Delgado

Msemaji huyo wa UNHCR amesema, “UNHCR inastaajabishwa na ripoti kwamba raia wa Msumbiji wamerejeshwa kwa nguvu na wanazuiwa kutafuta hifadhi. Tunatoa wito kwa pande zote kuruhusu raia wanaokimbia vurugu na mizozo, kutafuta ulinzi wa kimataifa, usalama na usaidizi, pamoja na kuheshimu na kushikilia kikamilifu haki ya kuvuka mipaka ya kimataifa kutafuta hifadhi.” 

Akifafanua zaidi kuhusu matukio hayo, Cheshirkov amesema huko Negomano, watu wameiambia UNHCR kwamba walikuwa wametenganishwa na wanafamilia wakati wanakimbia kutoka vijiji vyao nchini Msumbiji, ambapo wengine walitenganishwa baada ya kuwasili Tanzania.../

 

 

Tags