Nigeria kutumia vinasaba vya DNA kugundua magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7210-nigeria_kutumia_vinasaba_vya_dna_kugundua_magaidi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo ina mpango wa kutumia vinasaba yaani DNA kuwakamata magaidi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 17, 2016 04:16 UTC
  • Nigeria kutumia vinasaba vya DNA kugundua magaidi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo ina mpango wa kutumia vinasaba yaani DNA kuwakamata magaidi.

Shirika la habari la Xinhua limemnukuu Geoffrey Onyeama akisema hayo katika kikao cha pili cha usalama cha eneo la magharibi mwa Afrika huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria na kuongeza kuwa, serikali ya nchi hiyio iko tayari kuunda kituo maalumu cha uchunguzi wa DNA kwa ajili ya kuwagundua na kuwakamata wanamgambo wa Boko Haram nchini humo.

Amesema, hivi sasa kuna wakimbizi karibu milioni mbili nchini Nigeria na kwamba karibu watoto wadogo laki sita wenye umri wa chini ya miaka mitano wamepoteza wazazi wao. Amesema, uchunguzi wa vinasaba utasaidia sana kujua wasifu wa watoto hao na wazazi wao.

Kundi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi miaka sita iliyopita nchini Nigeria na limeshapelekea malefu ya watu kuuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi.

Raia wengi wa Nigeria wamelazimika kukimbilia nchi jirani kusalimisha roho zao kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Boko Haram.