Umoja wa Mataifa wataka juhudi zaidi kukabiliana na udhalilishaji wa kijinsia Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8293-umoja_wa_mataifa_wataka_juhudi_zaidi_kukabiliana_na_udhalilishaji_wa_kijinsia_kodivaa
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameishukuru serikali ya Ivory Coast kwa juhudi zake za kukabiliana na udhalilishaji wa kijinsia na kutaka juhudi zaidi ziongezwe katika uwanja huo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 02, 2016 04:07 UTC
  • Umoja wa Mataifa wataka juhudi zaidi kukabiliana na udhalilishaji wa kijinsia Kodivaa

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameishukuru serikali ya Ivory Coast kwa juhudi zake za kukabiliana na udhalilishaji wa kijinsia na kutaka juhudi zaidi ziongezwe katika uwanja huo.

Shirika la habari la Xinhua limemnukuu Bi Zainab Hawa Bangura ambaye ni mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya migogoro na udhalilishaji wa kijinsia, akisema hayo mwishoni mwa ziara yake ya siku tatu nchini Kodivaa.

Umoja wa Mataifa umesema, serikali ya Ivory Coast imepiga hatua nzuri katika kupambana na udhalilishaji wa kijinsia na jinai dhidi ya wanawake.

Zainab Hawa Bangura, ameongeza kuwa, jeshi na serikali ya Kodivaa imechukua hatua za maana za kuzuia kutokea jinai kama hizo nchini humo.

Mgogoro wa uchaguzi katika miaka 2010 na 2011 ulisababishia madhara makubwa Ivory Coast na kupelekea watu elfu tatu kuwa wahanga wa machafuko hayo ambayo yaliambatana na jinai kadhaa za udhalilishaji wa kijinsia.