Ikhwanul Muslimin 19 wahukukiwa kifungo cha maisha jela, Misri
-
Ikhwanul Muslimin
Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifungo cha maisha jela wanachama 19 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.
Wanachama hao 19 wa Ikhwanul Muslimin walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za kukuchochea machafuko na kufunga mabarabara.
Wakati wa kutolewa hukumu hiyo askari usalama wa Misri walizingira mahakama hiyo. Jumapili iliyopita mahakama ya kijeshi ya Alexandria pia iliwahukumu kifo wafuasi wengine 8 wa rais akiyeondolewa madarakani wa nchi hiyo, Muhammad Morsi. Hukumu hiyo sasa imetumwa kwa Mufti Mkuu wa Misri, Shawki Ibrahim Abdel-Karim Allam kwa ajili ya kupasishwa ingawa maoni yake si lazima kufuatwa na vyombo vya mahakama.
Muhammad Morsi, rais wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kwa njia za kidemokrasia aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo mwaka 2013 na kuswekwa jela na maelfu ya wafuasi wake wametiwa nguvuni na mamia ya wengine kuhukumiwa adhabu ya kifo.