Rwanda yatoa kipaumbele katika kuzihamisha kaya zilizokumbwa na maafa baada ya mafuriko
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i97396-rwanda_yatoa_kipaumbele_katika_kuzihamisha_kaya_zilizokumbwa_na_maafa_baada_ya_mafuriko
Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa inatoa kipaumbele kwa suala la kuhamisha kaya za maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko ya wikii iliyopita katika mikoa kdhaa ya Kaskazini na Magharibi mwa nchi hiyo.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
May 15, 2023 11:04 UTC
  • Rwanda yatoa kipaumbele katika kuzihamisha kaya zilizokumbwa na maafa baada ya mafuriko

Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa inatoa kipaumbele kwa suala la kuhamisha kaya za maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko ya wikii iliyopita katika mikoa kdhaa ya Kaskazini na Magharibi mwa nchi hiyo.

Mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita zilisababisha vifo vya  watu 137 na majeruhi wengine wengi katika mikoa ya kaskazini, magharibi na kusini mwa Rwanda. 

Tangu mvua kubwa zinyeshe huko Rwanda na kusababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko makubwa mapema mwezi huu, serikali ya nchi hiyo tayari imechukua hatua kadhaa za dharura, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha kwenye makazi salama  raia walioathiriwa na mafuriko..

Serikali ya Rwanda aidha imekusanya zaidi ya faranga milioni 10 kuwasaidiai watu waliokumbwa na mafuriko na maporomoko ya udongo. Serikali ya Kigali imetoa kipaumbele zaidi kwa suala la kuhamisha kaya 19,000 zinazoishi katika maeneo hatarishi. 

Alain Mukurarinda Naibu Msemaji wa Serikali ya Rwanda ameeleza mipango ya kitaifa ya ujenzi mpya wa maeneo yaliyoathiriwa na maafa hayo ya kimaumbile. 

Mafuriko ya Rwanda

Tabia nchi ya milima ya Rwanda inaifanya nchi hiyo ikabiliwe zaidi na mafuriko na maporomoko ya udongo ikilinganishwa na nchi nyingine. Watu waliohamishwa na kupelekwa kwenye makazi mapya wanaeleza jinsi maisha yao yalivyoboreka, na kusisitiza haja ya mabadiliko ya fikra miongoni mwa wananchi wanaosita kuhama kutoka maeneo yenye hatari kubwa kwenda maeneo salama.