-
Je Sudan Kusini ndio kituo kipya cha mpango wa kuwahamisha Wagaza kwa lazima?
Aug 14, 2025 00:09Chombo kimoja cha habari cha lugha ya Kiebrania kimetangaza kuwa, huku mashambulizi na vita katika Ukanda wa Gaza vikiendelea, Israel inafanya mazungumzo na Sudan Kusini, Indonesia, Libya, Ethiopia na nchi nyingine kadhaa za Kiafrika ili kuwapokea wakaazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Al-Burhan asisitiza kutoshirikishwa RSF katika mustakabali wa Sudan
Aug 13, 2025 07:30Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan, Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan, amesisitiza kuwa, Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) hakitakuwa na nafasi katika mustakabali wa nchi hiyo.
-
Al-Sisi: Misri haitafumbia macho haki yake ya maji
Aug 13, 2025 03:46Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, amesema kwamba mtu yeyote anayedhani kwamba Misri itafumbia macho haki yake ya kunufaika na maji ya Mto Nile anakosea.
-
Mapigano makali yaibuka tena kati ya jeshi la Kongo na M23
Aug 12, 2025 23:00Mapigano makali yameibuka baina ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Kundi la waasi wa M23, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi uliopita wa Julai.
-
RSF yashambulia kambi ya Abu Shouk Darfur Kaskazini
Aug 12, 2025 22:59Wanamgambo wa RSF wameishambulia kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk katika mkoa wa Darfur Kaskazini na kusababisha mauaji ya watu 40 huku wengine 19 wakijeruhiwa vibaya.
-
Rwanda yalaani ripoti ya Umoja wa Mataifa kwamba ilisaidia waasi wa M23 kuua raia
Aug 12, 2025 09:30Serikali ya Rwanda imelaani ripoti ya umoja wa Mataifa ya wiki iliyopoita, kuwa jeshi lake lililisaidia kundi la waasi wa M23 kuwauwa mamia ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Maandamano makubwa nchini Tunisia na Morocco kupinga vita na kuzingirwa Gaza
Aug 12, 2025 09:27Mamia ya Waafrika kaskazini mwa Afrika kwa mara nyingine tena wamejitokeza mitaani kuelezea upinzani wao dhidi ya vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza na siasa za kuwalazimishia njaa wakazi wa ukanda huo.
-
Gachagua amshambulia vikali Raila, asema hula peke yake akawakumbuka wafuasi wakati wa uchaguzi
Aug 12, 2025 04:12Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amemshambulia vikali kwa maneno kinara wa chama cha ODM Raila Odinga akimuelezea kuwa ni mwanasiasa anayewania urais bila kuutaka wadhifa huo.
-
Wanajeshi wa Somalia waliokula njama na Al Shabab ya kumuua kamanda wa kikosi chao wanyongwa
Aug 12, 2025 03:27Wanajeshi wawili wa Somalia waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kula njama na kundi la kigaidi la Al Shabab ya kumuua kamanda wa kikosi chao walitekelezewa hukumu yao jana Jumatatu. Hayo ni kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo.
-
Waasi wa M23 wakanusha maadai ya kuwauwa raia katika jimbo la Kivu Kusini
Aug 11, 2025 23:07Kundi la waasi wa M23 wanaodhibiti maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekanusha madai ya kuwauwa raia katika jimbo la Kivu Kusini pamoja na madai ya kuajiri askari watoto.