-
Kuondoa jeshi la Ufaransa nchini Senegal ni kikwazo kwa sera ya nje ya Paris barani Afrika
Jul 28, 2025 08:44Kuondoka kwa vikosi vya jeshi la Ufaransa katika kambi ya mwisho ya nchi hiyo huko Senegal na matamshi mbayo hayajawahi kutolewa hapo kabla ya afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Paris kwamba usalama wa Afrika Magharibi si muhimu kwa Ufaransa, kunadhihirisha kushindwa kwa sera ya muda mrefu ya ukoloni katika Bara la Afrika.
-
Sudan yaalaani tamko la RSF la kutangaza serikali nyingine nchini humo
Jul 28, 2025 03:52Serikali ya Sudan imelaani tangazo la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) la kuundwa serikali sambamba na kulitaja kuwa ni "ushahidi wa kushindwa na kusambaratika kwa kundi hilo."
-
Wasiwasi watanda, magaidi wakilenga tena kambi za polisi wa Kenya, Lamu
Jul 28, 2025 03:50Vikosi vya kulinda usalama msituni Boni, Kaunti ya Lamu nchini Kenya, vimezidisha msako dhidi ya magaidi wanaohusishwa na kundi la Al-Shabaab, baada ya jaribio jingine la kuvamia kambi ya polisi wa GSU.
-
Ramaphosa: Afrika Kusini imeshtushwa na njaa ya makusudi dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza
Jul 28, 2025 00:57Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameeleza kusikiitishwa sana na hali ya sasa ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza akisema kuwa raia hao "wanasumbuliwa na njaa ya makusudi" waliyosababishiwa na dola baguzi la Israel.
-
Tume ya Uchaguzi ya Cameroon yamzuia kugombea urais mshindani mkuu wa rais Biya
Jul 27, 2025 06:26Tume ya uchaguzi ya Cameroon, ELECAM, imetangaza kuwa mwanasiasa wa upinzani Maurice Kamto amezuiliwa kushiriki katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais wa Oktoba 12.
-
Watu karibu 45 wafariki Nigeria katika ajali ya boti na mapigano ya kikabila
Jul 27, 2025 03:41Takriban watu 27 wamepoteza maisha baada ya boti ya abiria kuzama katika Mto Niger, jimbo la Kogi nchini Nigeria. Boti hiyo ilikuwa imebeba takriban abiria 200 waliokuwa wakielekea sokoni kutoka jimbo la Kogi kwenda jimbo jirani la Niger, ilipozama siku ya Alhamisi jioni.
-
Umoja wa Afrika wakaribisha uamuzi wa Ufaransa wa kulitambua rasmi taifa la Palestina
Jul 26, 2025 23:44Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, amekaribisha tangazo la Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, la nia yake ya kulitambua rasmi Taifa la Palestina ifikapo Septemba mwaka huu.
-
Congo DR : M23 yatishia kususia mchakato wa amani kama wafungwa hawataachiliwa
Jul 26, 2025 23:04Kundi la waasi wa M23, ambalo linadhibiti maeneo mengi ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limetishia kususia mchakato wa amani unaoendelea sasa kutokana na suala la kuachiliwa kwa wafungwa jambo ambalo Kinshasa inachelewa kufanya.
-
Wanajeshi 4, magaidi 18 wauawa katika mapigano baada ya walinda amani wa Somalia na AU kuzima shambulio la al-Shabaab
Jul 26, 2025 08:21Wanajeshi wanne wameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika mapigano na kundi la kigaidi la al-Shabaab baada ya shambulio lao kuzimwa na jeshi la Somalia katika eneo la Lower Shabelle ambapo magaidi 18 wameuawa.
-
Uchaguzi Tanzania 2025: Watanzania kupiga kura Oktoba 29
Jul 26, 2025 08:07Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (INEC) Tanzania imetangaza kuwa, uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2025), utakaohusisha nafasi ya Rais, wabunge na madiwani, utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025.