-
Magaidi 18 wa Al Shabaab waangamizwa katika mapigano makali Somalia
Jul 26, 2025 04:09Magaidi wasiopungua 18 wa kundi la Al Shabaab waangamizwa nchini Somalia katika mapigano makali baina yao na jeshi la nchi hiyo likishirikana na askari wa Umoja wa Afrika.
-
Wasudani zaidi ya milioni 1.3 waliokimbia makazi yao wamerejea nyumbani
Jul 25, 2025 23:00Licha ya mzozo unaoendelea kote Sudan, zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni moja waliokimbia vita wamerejea katika makazi yao, pamoja na wengine 320,000 waliorejea nchini wakitokea Misri na Sudan Kusini tangu waliopata hifadhi katika nchi hizo mwaka jana.
-
Bunge la Libya: Jamii ya kimataifa ivunje ukimya wake wa kufedhehesha kuhusu Gaza
Jul 25, 2025 22:57Katika taarifa yake ya jana Ijumaa, Bunge la Libya limeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua haraka na madhubuti dhidi ya sera ya njaa inayotekelewa na Israel dhidi ya wanawake na watoto madhulumu wa Palestina huko Gaza.
-
Mkutano wa Usalama wa Mtandao Barani Afrika wafunguliwa Niamey, Niger
Jul 25, 2025 07:26Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao ujulikanao kama “Kupeana Mkono kwa Ajili ya Mustakabali wa Kidijitali” umefunguliwa rasmi jijini Niamey, mji mkuu wa Niger, ukiwaleta pamoja wadau kutoka pembe mbalimbali za bara la Afrika.
-
IPOA yafichua: Polisi wa Kenya waliua watu 65 katika maandamano Juni, Julai
Jul 25, 2025 02:14Ripoti mpya ya Mamlaka Huru ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA) imefichua kwamba watu 65 walipoteza maisha, 41 kati yao kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi, huku raia 342 wakijeruhiwa vibaya wakati wa maandamano ya Juni 25 na Julai 7 mwaka huu dhidi ya serikali ya Rais William Ruto wa Kenya.
-
Marais wawili wa zamani ni miongoni mwa wanaowania urais Malawi
Jul 24, 2025 23:18Wagombea zaidi ya 20 nchini Malawi, wakiwemo marais wawili wa zamani, ni miongoni mwa wanasiasa wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi ujao.
-
Umoja wa Mataifa: Maafisa wetu wamezuiwa na M23 kuingia mashariki ya Congo
Jul 24, 2025 23:08Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, wataalamu wake walizuiwa na waasi wa M23 kufanya uchunguzi wao katika ngome wanazoshikilia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
-
Mlipuko wa kipindupindu wauwa watu 13 katika jimbo la Niger, nchini Nigeria
Jul 24, 2025 07:01Takriban watu 13 wamefariki dunia na wengine 239 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kuenea katika wilaya sita za jimbo la Niger katikati mwa Nigeria. Taarifa hii imetolewa na mamlaka husika katika jimbo la Niger.
-
Maisha ya watu milioni 1.3 Nigeria yako hatarini baada ya WFP kusitisha misaada
Jul 24, 2025 03:19Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa litalazimika kusitisha msaada wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 katika eneo lililokumbwa na machafuko zaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwishoni mwa mwezi huu wa Julai kutokana na hifadhi yake ya chakula na virutubisho vya lieshe kumalizika.
-
Sheikh Mkuu wa al-Azhar atoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kuiokoa Gaza
Jul 23, 2025 23:19Sheikh Mkuu wa al-Azhar ya Misri ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa kuokoa maisha ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza kutokana na kifo cha njaa.