-
Ukatili wa Polisi Dhidi ya Waandamanaji wa Siku ya Kimataifa Quds Nchini Nigeria
Mar 31, 2025 23:09Katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaliyofanyika nchini Nigeria Ijumaa kwa kushirikisha mamia ya Waislamu na wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo – kwa lengo la kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina na kulaani uhalifu wa utawala wa Kizayuni wa Israel– maafisa wa polisi wa Nigeria walifyatua risasi dhidi ya waandamanaji. Tukio hilo lilisababisha waandamanaji wasiopungua 18 kuuawa shahidi, wengine kujeruhiwa, na wengi kukamatwa.
-
Baraza la Usalama lalaani kushambuliwa walinda amani wa UN nchini CAR
Mar 31, 2025 08:21Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shambulizi lililofanywa dhidi ya askari wa kulinda amani wa umoja huo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Askari mmoja raia wa Kenya ameuawa kwenye shambulio hilo.
-
Makumi ya wanajeshi na raia wauawa katika shambulizi mashariki mwa Burkina Faso
Mar 31, 2025 07:52Makumi ya wanajeshi na raia kutoka makundi yanayoliunga mkono jeshi la Burkina Faso wameuawa katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.
-
Gabon yaanza kampeni ya urais kabla ya uchaguzi wa Aprili 12
Mar 30, 2025 23:10Kampeni za uchaguzi wa urais nchini Gabon zimeanza rasmi siku ya Jumamosi na zitaendelea hadi Aprili 11. Upigaji kura utafanyika Aprili 12.
-
Nigeria yalaaniwa kwa kukandamiza waandamanaji wa Siku ya Quds
Mar 30, 2025 07:42Baraza la Uratibu wa Tablighi ya Kiislamu la Iran limetoa taarifa ya kulaani ukandamizaji waliofanyiwa Waislamu wa Nigeria wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kuandika: "Ukandamizaji na kumwagwa damu za waandamanaji wa Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Nigeria na kuuawa shahidi kidhulma Waislamu 18 waliokuwa kwenye saumu ya Ramadhani kunaonesha hofu ya watawala wa Nigeria kuhusu mwamko wa Waislamuj na nafasi ya kiistratijia ya Siku ya Kimataifa ya Quds duniani."
-
Wataalamu watoa mwito wa mageuzi Afrika chini ya urais wa G20 wa Afrika Kusini
Mar 30, 2025 07:36Wataalamu na watunga sera waliohudhuria mkutano kuhusu vipaumbele vya Afŕika chini ya Urais wa Afrika Kusini wa Kundi G20 wamesisitizia haja ya kuyapa kipaumbele mageuzi muhimu ambayo yatasaidia ustawi na maendeleo ya Afŕika.
-
Al Burhan apinga mazungumzo Sudan, atangaza ushindi kamili
Mar 30, 2025 07:34Abdel Fattah Al-Burhan, Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Sudan SAF, amepinga vikali mazungumzo ya aina yoyote ile na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF na kutangaza ushindi kamili dhidi ya vikosi hivyo.
-
Guinea yatoa msamaha uliobua utata kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Dadis Camara
Mar 29, 2025 23:08Katika uamuzi wa kutatanisha, kiongozi wa utawala wa kijeshi wa Guinea, Jenerali Mamadi Doumbouya, ametoa msamaha wa rais kwa mtawala wa zamani wa kijeshi Moussa Dadis Camara.
-
Watu wasiopungua 20 wameuawa katika hujuma ya wanajeshi wa Nigeria dhidi ya maandamano ya Siku ya Quds, Abuja
Mar 29, 2025 07:46Makumi ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina wameuawa na wengine kujeruhiwa wakati askari usalama walipofyatua risasi kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
-
Mijumuiko ya Siku ya Quds yafanyika nchini Kenya
Mar 29, 2025 04:33Maandamano na mijumuiko ya siku ya kimataifa ya Quds imefanyika maeneo mbali mbali nchini Kenya katika ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.