-
Bunge la Algeria lakata uhusiano na Seneti ya Ufaransa kutokana na Sahara Magharibi
Feb 27, 2025 04:20Baraza la Taifa la Algeria, ambalo ni baraza la juu la bunge, lilisitisha uhusiano wake na Seneti ya Ufaransa siku ya Jumatano kufuatia ziara ya spika wa seneti hiyo katika eneo la Sahara Magharibi linalozozaniwa.
-
Waislamu wa Ghana wamuenzi na kumuomboleza Sayyid Hassan Nasrullah
Feb 26, 2025 23:47Jumuiya ya Waislamu wa Ghana mjini Accra imefanya hafla ya kumbukumbu ya Sayyed Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, ambaye walimtukuza kama shahidi wa Uislamu na ubinadamu.
-
Vikosi vya serikali Sudan Kusini vyashambulia kwa bomu kambi ya kiongozi wa upinzani Riek Machar
Feb 26, 2025 23:46Hali ya wasiwasi inaongezeka tena nchini Sudan Kusini licha ya wito wa kuheshimiwa makubaliano ya amani.
-
Somalia na Umoja wa Afrika wakubaliana kuhusu wanajeshi watakaojumuishwa katika kikosi kipya
Feb 26, 2025 23:45Serikali kuu ya Somalia na Umoja wa Afrika wamekubaliana kuhusu idadi ya wanajeshi kutoka nchi mbalimbali watakaohudumu katika kikosi kipya cha Umoja wa Afrika.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda: 'Umoja wa Mataifa sio Biblia', tutaendelea kuzipinga ripoti zake
Feb 26, 2025 09:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amesema, Umoja wa Mataifa sio Biblia, na kwamba nchi yake itapinga ripoti zake za madai kwamba Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mashariki mwa nchi hiyo.
-
Operesheni ya Jeshi la Somalia yaua magaidi 70 wa Al-Shabaab katika jimbo la Hirshabelle
Feb 26, 2025 08:12Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza kuwa vikosi vya jeshi vikishirikiana na vikosi vingine vya ndani vimewaua wanamgambo wapatao 70 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika operesheni ya mashambulizi viliyotekeleza jana Jumanne katika maeneo kadhaa ya jimbo la Hirshabelle kusini mwa katikati ya nchi hiyo.
-
Gachagua amuomba Raila kuungana na wapinzani wa Rais Ruto, amuahidi urais wa Kenya mwaka 2027
Feb 26, 2025 02:39Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amesema kwamba anaweza kumfanya kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwa rais wa Kenya iwapo atakubali kuungana naye na vigogo wengine wa upinzani.
-
DRC Yasitisha Usafirishaji wa Kobalti kwa Miezi Minne
Feb 25, 2025 22:51Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesitisha usafirishaji wa kobalti kwa miezi minne ili kudhibiti usambazaji wa kobalti kwenye soko la kimataifa, ambalo kwa sasa linakabiliwa na upitilivu wa bidhaa hiyo. Hali hii imesababisha kushuka kwa bei kwa mfululizo.
-
Uwezekano wa kutokea vita katika eneo la Maziwa Makuu
Feb 25, 2025 10:21Huku vikosi vya waasi wa M23 vikiendelea kusonga mbele katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeongeza hatari ya kutokea vita vya pande zote katika eneo la Maziwa Makuu Afrika.
-
EAC na SADC zawateua marais wastaafu wa Afrika kusuluhisha mzozo wa Kongo DR
Feb 25, 2025 06:15Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC zimewateua Uhuru Kenyatta kutoka Kenya, Olusegun Obasanjo kutoka Nigeria, na Hailemariam Desalegn kutoka Ethiopia kuongoza mazungumzo ya kutatua mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).