-
Sudan yatishia kulipiza kisasi dhidi ya Kenya kwa kuwa mwenyeji wa RSF
Feb 25, 2025 02:30Serikali ya Sudan jana Jumatatu iliapa kuchukua hatua kali dhidi ya Kenya kutokana na Nairobi kuwa mwenyeji wa kikao cha wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Viongozi wa Libya na Somalia wajadiliana ushirikiano katika uwekezaji na elimu
Feb 25, 2025 02:28Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya, Mohamed Menfi, amesisitizia umuhimu wa kuweko ushirikiano baina ya nchi yake na Somalia katika nyuga tofauti. Mwito huo aliutoa jana Jumatatu katika mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari baina yake na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliyeko ziarani nchini Libya.
-
Hujuma za waasi mashariki mwa Kongo zimeuwa watu 7,000 mwaka huu
Feb 24, 2025 23:00Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa watu zaidi ya elfu saba wameuawa mwaka huu wakati waasi wa kundi la M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiteka miji kadhaa katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa Kongo.
-
Senegal yasaini makubaliano ya amani na kundi linalopigania kujitenga eneo la Casamance
Feb 24, 2025 22:55Serikali ya Senegal na harakati kwa jina la Movement of Democratic Forces of Casamance (MFDC); kundi la waasi linalopigania kujitenga eneo la kusini mwa Senegal la Casamance wametia saini makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo, na hivyo kumaliza moja ya migogoro mikongwe zaidi barani Afrika, ambayo imedumu kwa miongo minne.
-
Waasi wa DRC watangaza kuwa tayari kwa usitishaji mapigano
Feb 24, 2025 08:53Muungano wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Alliance Fleuve Congo (AFC), unaojumuisha waasi wa M23, umetangaza kuwa tayari kushiriki mazungumzo na serikali ili kusitisha mara moja mapigano mashariki mwa nchi, msemaji wa kundi hilo amesema.
-
Jeshi la Sudan lakomboa mji mpya, latangaza mafanikio dhidi ya waasi wa RSF
Feb 24, 2025 08:52Jeshi la Sudan limekomboa mji mwingine kusini mwa Sudan siku ya Jumapili, ikiwa ni mafanikio mapya katika mapambano dhidi ya kundi la waasi wa kundi la RSF.
-
UNHCR: Tunahitaji dola milioni 40 kusaidia wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Feb 24, 2025 03:44Wakati waasi wa M23 wakiendelea kusonga mbele katika mkoa wa Kivu Kaskazini na Kusini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeaomba zaidi ya dola milioni 40 kusaidia watu waliokimbia makazi yao katika mikoa hiyo mawili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na katika nchi jirani.
-
Harakati ya Kiislamu Nigeria yawaenzi na kuwaomboleza viongozi wa muqawama
Feb 24, 2025 03:43Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria katika Jimbo la Kano imewaenzi na kuwaomboleza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyed Hassan Nasrullah na Mkuu wa zamani wa Baraza la Utendaji la harakati hiyo, Sayyed Hashem Safieddine, waliouawa shahidi katika shambulio la anga la Israel huko Beirut.
-
Joseph Kabila: Uongozi mbaya wa Rais Tshisekedi umezidisha mzozo mashariki mwa DRC
Feb 24, 2025 03:42Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amesema kuuwa, uongozi mbaya wa mrithi wake, Rais Felix Tshisekedi umechangia pakubwa kuzidisha mzozo mashariki mwa nchi hiyo.
-
Mkutano wa kikanda kuhusu mapigano Kongo DR kufanyika leo Dar es Salaam
Feb 23, 2025 23:36Tanzania leo Jumatatu, inatazamiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda, kufuatilia matukio ya nyanjani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuchukua hatua zinazohitajika za kukabiliana na mgogoro huo.