-
Uhusiano wa kidiplomasia wa Kenya na Sudan matatani baada ya Nairobi kuwa mwenyeji wa RSF
Feb 20, 2025 04:10Kenya na Sudan huenda zikaingia katika mgogoro wa kidiplomasia baaada ya Nairobi kuwa mwenyeji wa mkutano wa wanamgambo wa RSF wanaopigana na serikali ya Khartoum.
-
Indhari ya MSF kuhusu mapigano ya silaha na uporaji mashariki mwa DRC
Feb 19, 2025 23:08Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka (MSF) limetoa tahadhari kuhusu mapigano ya silaha na uporaji katika eneo lililoathiriwa na vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Uganda yasema imeweza kudhibiti mlipuko wa Ebola
Feb 19, 2025 23:05Uganda imesema imeweza "kudhibiti" mlipuko wa hivi karibuni wa virusi vya Ebola aina ya Sudan, ambao ulithibitishwa na Wizara ya Afya mwishoni mwa Januari.
-
Sudan kukabiliana na watakaojaribu kuunda serikali nyingine
Feb 19, 2025 08:39Mjumbe wa Baraza Kuu la Sudan amesema serikali ya nchi hiyo "itapambana na yeyote anayetaka kuanzisha serikali nyingine" katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Waasi wa Tuareg: Jeshi la Mali limewaua raia 24 kaskazini mwa nchi
Feb 19, 2025 08:33Muungano wa waasi wa Tuareg huko kaskazini mwa Mali umewatuhumu wanajeshi wa nchi hiyo kwa kuwaua raia 24 waliokuwa wakisafiri kuelekea kaskazini mwa Algeria kutoka mji wa Gao, huku jeshi likiripoti habari ya kujiri mapigano katika eneo hilo.
-
Uganda yatuma vikosi zaidi nchini DRC, yathibitisha kuwa wanajeshi wake wameingia Bunia
Feb 19, 2025 02:59Msemaji wa Jeshi la Uganda Brigedia Jenerali Felix Kulayigye amethibitisha kuwa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo (UPDF) limeingia kwenye eneo la Bunia, ambalo ni makao makuu ya jimbo la Ituri, sehemu muhimu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
-
UNHCR: Karibu wakimbizi 15,000 kutoka DRC wameingia Burundi
Feb 18, 2025 23:44Zaidi ya watu 10,000 hadi 15,000 wamevuka mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuingia Burundi katika siku chache zilizopita wakikimbia mapigano yanayoshadidi mashariki mwa DRC.
-
Afrika Kusini yapata msaada kutoka China baada ya vikwazo vya Trump
Feb 18, 2025 23:18Marekani haikujibu maombi ya Afrika Kusini ya kujadili kupunguzwa kwa misaada ya Rais wa Marekani Donald Trump, na kufuatia jambo hilo China imeahidi kuipa Pretoria msaada unaohitajika.
-
Katibu Mkuu wa UN: Hakuna kisingizio cha kuikosesha Afrika kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama
Feb 18, 2025 10:12Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, hakuna kisingizio cha kuifanya Afrika iendelee kuwa haina uwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Jeshi la Sudan lasonga mbele katika mji mkuu Khartoum na mji wa Bahri
Feb 18, 2025 10:11Jeshi la Sudan limetangaza kuwa linaendelea kusonga mbele katika mji mkuu Khartoum na mji wa Bahri ulioko kaskazini mwake, na kutwaa udhibiti wa vitongoji kadhaa.