-
"Maharamia" warejea kwa nguvu Somalia, wateka nyara meli ya uvuvi
Feb 12, 2025 03:08Watu wanaoshukiwa kuwa mo maharamia wameteka nyara meli ya uvuvi iliyokuwa na bendera ya Yemen karibu na Eyl, kaskazini mwa Somalia.
-
Mvutano wazuka kati ya Misri na Marekani baada ya tishio la Trump; el Sisi 'huenda akaashirisha' ziara ya Washington
Feb 11, 2025 10:46Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi huenda akaahirisha ziara yake iliyokuwa imepangwa mjini Washington, kama ishara ya mkwamo mkubwa wa kidiplomasia wakati huu kukiwa na mvutano unaoongezeka kati yake na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mgogoro wa Gaza na vitisho vya kukata misaada ya Washington kwa serikali ya Cairo.
-
Wanamgambo wa CODECO washambulia na kuuwa zaidi ya watu 35
Feb 11, 2025 10:20Wanamgambo wenye silaha wamewaua zaidi ya raia 35 na kuwajeruhi wengine kadhaa, katika shambulio lililotokea usiku wa Jumatatu katika vijiji vya baadhi vya jimbo la Ituri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Umoja wa Mataifa walishutumu kundi la RSF kwa kuzuia misaada inayopelekwa Darfur, Sudan
Feb 11, 2025 03:22Umoja wa Mataifa umevishutumu Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF vya Sudan kwa kuzuia msaada katika eneo linalokabiliwa na njaa la Darfur magharibi mwa nchi hiyo.
-
Wafanyabiashara Nigeria wataka kususiwa bidhaa za Israel
Feb 10, 2025 07:56Kundi moja la wajasiriamali wadogo na wa kati nchini Nigeria, limeandaa mkutano wa siku mbili katika Jimbo la Kaduna la kaskazini magharibi mwa nchi, kujadili mikakati ya kibiashara na umuhimu wa kususia bidhaa za Israel, ili kuonyesha uungaji mkono kwa kadhia ya Palestina.
-
DRC yawapandisha kizimbani wanajeshi wake kwa kutoroka vita; inawatuhumu pia kwa ubakaji
Feb 10, 2025 03:52Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa wanajeshi wasiopungua 75 wanatazamiwa kufikishwa mahakamani leo Jumatatu wakikabiliwa na shtaka la kuwakimbia wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika jimbo la Kivu ya Mashariki.
-
Bunge la Afrika Mashariki lasimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kwa sababu za kifedha
Feb 10, 2025 03:30Bunge la nchi za Afrika Mashariki, EALA limetangaza kuwa limesimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kutokana na changamoto za kifedha, zilizosababishwa na baadhi ya nchi wanachama kushindwa kulipa michango yao ya fedha.
-
Libya yagundua makaburi mawili ya halaiki yenye miili ipatayo 50 ya wahajiri na wakimbizi
Feb 10, 2025 03:29Mamlaka za Libya zimegundua miili ipatayo 50 kwenye makaburi mawili ya halaiki katika jangwa la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika maafa ya karibuni zaidi yaliyohusisha watu wanaotaka kufika Ulaya kupitia nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.
-
Vyombo vya habari Kenya vyazungumzia athari za ushindi wa Odinga kama mkuu wa Kamisheni ya AU
Feb 09, 2025 23:13Vyombo vya habari vya Kenya vimechapisha ripoti kuhusu athari za matokeo ya ushindi wa mgombea wa nchi hiyo, Raila Odinga, katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, unaotarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Afrika mjini Addis Ababa wiki ijayo, katika siasa za ndani nchini Kenya.
-
Wanasheria Tunisia: Kesi ya Instalingo ni njama ya Kisiasa ya kuwamaliza wapinzani wa serikali
Feb 09, 2025 23:12Maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya Tunisia katika kesi inayojulikama kama "Instalingo" yanaendelea kuibua hisia hasi kutoka kwa mawakili, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na timu ya utetezi kwa washtakiwa, ambao wanayataja maamuzi hayo kuwa yasiyo na mantiki wala msingi wa kisheria, na kwamba lengo lake ni kuwafutilia mbali wapinzani wa kisiasa wa serikali ya Tunis.