-
Mali: Tunawasaka wanamgambo wenye silaha waliouwa watu zaidi ya 25
Feb 09, 2025 23:11Jeshi la Mali limeahidi kuwasaka "magaidi" waliohusika na shambulio la kikatili dhidi ya msafara mkubwa uliokuwa ukielekea kwenye mgodi wa dhahabu nchini humo.
-
Suluhisho la kikanda ndiyo njia bora ya kumaliza mgogoro wa Kongo DR
Feb 09, 2025 07:17Wakuu wa nchi wanachama katika jumuiya mbili za kikanda za Mashariki na Kusini mwa Afrika, jana Jumamosi, wafanya mkutano wa aina yake katika mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam wakijaribu kutafuta suluhisho la kumaliza mgogoro wa mashariki mwa Kongo DR.
-
Ethiopia yaahidi kutumia fursa za biashara huria kutoa fursa zaidi barani Afrika
Feb 09, 2025 07:09Waziri wa Biashara na Ushirikiano wa Kikanda wa Ethiopia amesema kuwa, nchi yake ina nia thabiti ya kuhakikisha kunakuwepo utekelezaji madhubuti wa makubaliano ya Eneo Huria la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) ili kutoa fursa kubwa za soko la ndani ya bara pana na kubwa la hilo.
-
Bunge la Libya lalaani njama za Wazayuni za kuwahamisha watu wa Ghaza
Feb 09, 2025 07:07Bunge la Libya limelaani na kupinga njama za Marekani na Israel za kutaka kuwahamisha wananchi wa Ghaza na kuwapeleka sehemu nyingine nje ya ardhi zao za jadi za Palestina.
-
Waafrika Kusini 'weupe' wakataa 'ofa' ya kuwa wakimbizi Marekani
Feb 09, 2025 03:42Raia wa Afrika Kusini wenye asili ya Uholanzi na nchi nyingine za Ulaya wamepuuzilia mbali mwito wa Rais Donald Trump, wa kwenda kuwa wakimbizi nchini Marekani, kwa madai ya kubaguliwa nchini Afrika Kusini.
-
'Baba wa Taifa' wa Namibia aaga dunia akiwa na miaka 95
Feb 09, 2025 03:40Rais wa kwanza wa Namibia huru, Sam Nujoma, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Windhoek.
-
Jumuiya za SADC na EAC zataka kusitishwa mapigano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Feb 08, 2025 23:55Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC wametoa mwito wa kusitishwa mara moja mapigano mashariki mwa Jamhuuri ya Kidemokkrasia ya Congo.
-
UN: Mapigano yaendelea Kivu Kusini, watu wengi wahama makazi yao
Feb 08, 2025 22:56Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, wakati vita vikipungua katika mji wa Goma unaokaliwa kwa mabavu na waasi ambao UN inasema wanaungwa mkono na Rwanda, maafisa wake wa huduma za kibinadamu wamesema kuwa, mapigano yamepamba moto katika jimbo la Kivu Kusini na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao.
-
Ushiriki wa Nigeria katika BRICS ni muhimu, kwa nini?
Feb 08, 2025 22:51Uanachama wa Nigeria katika shirika la BRICS, kama "nchi mshirika" na yenye uchumi mkubwa zaidi katika bara la Afrika, ni suala muhimu na lenye taathira kwa bara hilo na mataifa yanayoinukia kiuchumi.
-
Rais Samia awataka viongozi wa kikanda kuupatia ufumbuzi mgogoro wa DRC
Feb 08, 2025 09:40Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa kikanda wa kutatua mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amewataka viongozi wa kikkanda kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo hharaka iwezekanavyo.