-
Uganda yatuma askari 1,000 zaidi mashariki mwa DRC
Feb 04, 2025 23:10Uganda imeripotiwa kutuma wanajeshi zaidi ya 1,000 wa ziada huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndani ya wiki moja iliyopita, karibu na eneo ambalo wanajeshi wa serikali ya Kinshasa wanapambana na waasi wa M23.
-
IOM: Vita vya Sudan vimeongeza idadi ya wakimbizi wa ndani Pembe ya Afrika
Feb 04, 2025 23:10Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema idadi ya wakimbizi wa ndani (IDP) katika Pembe ya Afrika iliongezeka hadi milioni 20.75 kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2024.
-
Muungano wa waasi wa mashariki mwa Kongo likiwemo kundi la M23 watangaza kusitisha mapigano
Feb 04, 2025 04:00Muungano kwa jina la The Alliance Fleuve Congo; muungano wa waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaolijumuisha pia kundi la waasi wa M23 umetangaza kusitisha mapigano kuanzia leo Jumanne Februari 4.
-
Watu 44 wauawa katika shambulio la waasi wa SPLM-N huko Kordofan Kusini
Feb 04, 2025 03:59Maafisa wa Sudan wametangaza kuwa watu wasiopungua 44 wameuawa na 28 kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa harakati ya SPLM-N inayoongozwa na Abdelaziz al Hilu katika makao makuu ya jimbo la Korofan Kusini kusini mwa Sudan.
-
Ramaphosa: Afrika Kusini haitajitoa katika kikosi cha kulinda amani Kongo
Feb 03, 2025 23:20Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahidi kuendelea kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya wananchi wa Afrika Kusini kutoa wito wa kuondoka Kongo wanajeshi wa nchi hiyo kufuatia vifo vya walinda amani 14 wa Afrika Kusini.
-
67 wauawa katika shambulizi la wanamgambo kwenye mji wa El Fasher, magharibi mwa Sudan
Feb 03, 2025 23:15Jeshi la Sudan SAF limetangaza kuwa, takriban watu 67 waliuawa Jumapili katika shambulizi la mizinga lililofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini la magharibi mwa Sudan.
-
Ramaphosa apinga bwabwaja mpya za rais wa Marekani, asema hakuna ardhi iliyotwaliwa na Afrika Kusini
Feb 03, 2025 06:59Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini leo Jumatatu amepinga bwabwaja na madai ya rais wa Marekani Donald Trump na kusema kuwa Pretoria haijawahi kunyang'anya ardhi yoyote ile.
-
Watu 54 wauawa na 158 wajeruhiwa katika shambulio la kijeshi sokoni huko Omdurman nchini Sudan
Feb 03, 2025 06:58Idadi ya watu waliouawa kutokana na kushambuliwa kwa makombora na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) siku ya Jumamosi kwenye soko lenye watu wengi huko Omdurman, kaskazini mwa mji mkuu wa Sudan Khartoum, imeongezeka na kukfikia 54.
-
Jeshi la Tanzania lathibitisha kuuwa askari wake wawili DRC, Rwanda yakaribisha kujadiliwa mzozo
Feb 03, 2025 02:23Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza kuwa, wanajeshi wake wawili ni miongoni mwa askari 20 wa kulinda amani waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Burundi yaonya kuhusu kutokea vita vikubwa vya kikanda
Feb 02, 2025 23:56Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameonya kuwa mzozo unaoongezeka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaweza kuzusha vita vikubwa zaidi vya kikanda katika eneo la Maziwa Makuu.