-
Paul Biya (92) atangazwa mshindi wa kiti cha urais Cameroon
Oct 27, 2025 23:43Baraza la katiba la Cameroon limemtangaza Rais aliyeko madarakani Paul Biya kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa karibu asilimia 54% ya kura.
-
Mpinzani mkuu Ivory Coast akubali kushindwa huku matokeo ya awali yakionyesha rais Ouattara anashinda
Oct 27, 2025 08:46Waziri wa zamani wa biashara wa Ivory Coast, Jean-Louis Billon, amekubali kushindwa na Rais aliyepo madarakani, Alassane Ouattara, katika uchaguzi wa urais wa taifa hilo, kufuatia matokeo ya awali yanayoonyesha Ouattara akiongoza katika kura zilizohesabiwa.
-
Rais wa Namibia amfukuza kazi Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo
Oct 27, 2025 03:05Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah wa Namibia jana alimfukuza kazi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Viwanda, Natangwe Ithete.
-
Mgogoro wa mafuta nchini Mali wasababisha kufungwa shule kote nchini
Oct 27, 2025 02:51Mali imefunga shule nchini kote kwa muda wa wiki mbili kutokana na uhaba wa mafuta unaoendelea.
-
Wanamgambo wa RSF wadai kutwaa makao makuu ya jeshi la Sudan katika mji wa al Fasher
Oct 26, 2025 23:25Mapigano yalipamba moto jana Jumapili katika mji uliozingirwa wa al Fasher huko Sudan katika jimbo la Darfur Kaskazini, huku kundi la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) likidai kuiteka kambi ya jeshi la Sudan (SAF).
-
Zaidi ya mashtaka 1,500 yamefunguliwa Morocco baada ya maandamano ya Gen Z
Oct 26, 2025 08:30Asasi isiyo ya kiserikali ya Morocco imesema kwamba zaidi ya watu 1,500 walioshiriki katika maandamano yaliyoenea katika kona zote za Morocco wakidai huduma bora ya afya, elimu na kukomeshwa ufisadi, wamefunguliwa mashtaka na serikali. Maandamano hayo yalidumu kwa mwezi mzima.
-
AU yahimiza kuchukuliwa hatua madhubuti za kudhamini chakula Afrika
Oct 26, 2025 08:30Kamishna wa Kilimo, Maendeleo Vijijini, Uchumi wa Bluu na Mazingira Endelevu wa Umoja wa Afrika (AU), Moses Vilakati ametaka kuchukuliwe juhudi zaidi na zilizoratibiwa vyema kwenye bara zima la Afrika ili kushughulikia changamoto kubwa za usalama wa chakula barani humo.
-
Zimbabwe yatoa mwito wa kuondolewa vikwazo vya Magharibi bila ya masharti
Oct 26, 2025 08:29Jana Zimbabwe ilifanya maadhimisho ya Siku ya Kikanda ya Kupinga Vikwazo huko Harare, mji mkuu wa nchi hiyo. Wananchi wa Zimbwe wametaka kuondolewa vikwazo vya nchi za Magharibi bila ya masharti na kuruhusiwa taifa lao kufanikisha malengo yake ya ustawi wa kiuchumi.
-
Jeshi la Sudan lapambana na waasi wa RSF katika miji ya el-Fasher na Bara
Oct 26, 2025 04:35Mapigano yamezidi kushadidi maeneo kadhaa ya Sudan baada ya waasi wa RSF kuendeleza mashambulizi dhidi ya mji wa el-Fasher ulioko Kaskazini mwa Darfur, pamoja na mji wa Bara katika mkoa wa Kordofan Kaskazini.
-
Ethiopia na Somalia zaahidi amani katika eneo wakati wa Jukwaa la 11 la Tana
Oct 26, 2025 04:33Ethiopia na Somalia zimeithibitishia dunia dhamira yao ya kudumisha amani ya kikanda wakati wa Jukwaa la 11 la Tana ambalo limejadili jukumu la kimkakati la Pembe ya Afrika.