Mwandishi wa habari wa Marekani amwita Trump "mateka wa Netanyahu"
-
Carlson: Trump ni mtumwa wa Netanyahu
Mchambuzi wa Marekani, Tucker Carlson amemtaja Donald Trump kama mtu anayedhibitiwa kwa mbali na mateka wa Waziri Mkuu wa Israel katika vita vya Iran.
Tucker Carlson amemkosoa vikali Rais wa Marekani, Donald Trump katika mahojiano na "New York Times" na kusema kwamba hakuwa na chaguo lla kujiunga na utawala wa Israel katika kushambulia Iran. Amesema: Rais Trump ni "mtumwa" na "matekwa" wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na waungaji mkono wake nchini Marekani.
Tucker Carlson, ambaye ana ushawishi mkubwa katika harakati za kihafidhina za Marekani, hivi karibuni alimkosoa Donald Trump kwa njia isiyo ya kawaida, akitaja sera zake za kuingia vitani na Iran kuwa ni kinyume na kauli mbiu ya "Amerika Kwanza"; msimamo unaoonyesha mgawanyiko unaoongezeka miongoni mwa waungaji mkono wa chama cha Republican na ufafanuzi mpya wa vipaumbele vya sera za kigeni za Marekani.
Carlson, ambaye alikuwa muungaji mkono muhimu wa Donald Trump kwa miaka mingi, sasa amekuwa mmoja wa wakosoaji wake wakubwa, hasa kuhusu sera za kigeni. Katika matamshi yake ya karibuni, alisisitiza kwamba kuingia Marekani katika vita na Iran kulikuwa kinyume kabisa na ahadi za Trump za kukomesha vita visivyoisha vya Marekani.