-
Sauti za milio ya risasi zasikika karibu na kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Niger, Niamey
Aug 29, 2026 10:38Wakazi wa Niamey, mji mkuu wa Niger wameeleza kuwa milio za risasi zimesika usiku wa kuamkia leo Jumamosi karibu na kambi ya kijeshi katika uwanja wa ndege wa kimataifa ambao mwaka huu umeshambuliwa mara mbili na wanamgambo wanaobeba silaha.
-
Sudan yafuta marufuku ya kutoka nje Khartoum, mafuriko yameharibu makumi ya nyumba Kordofan Kusini
Aug 29, 2026 02:46Serikali ya Sudan imetangaza kufutwa marufuku ya kutoka nje katika jimbo la Khartoum baada ya karibu miaka miwili ya utekelezaji wake kutokana na vita kati ya Jeshi la Taifa na waasi wa Rapid Support Forces (RSF).
-
Ndejembi apitishwa kwa 100% kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aug 28, 2026 14:37Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limempitisha Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupata kura zote 324 zilizopigwa, sawa na asilimia 100.
-
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaanza kutoa chanjo ya Ebola
Aug 28, 2026 09:55Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni katika juhudi za kudhibiti mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa huo kuwahi kurekodiwa nchini humo.
-
Mwana wa rais wa Uganda atangaza nia ya kumrithi baba yake katika uchaguzi wa 2031
Aug 28, 2026 03:26Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni, amesema atagombea urais mwaka 2031.
-
WHO yathibitisha Uganda haina Ebola, ugonjwa huo unaendelea kuenea Kongo
Aug 27, 2026 11:57Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha kumalizika mlipuko wa Ebola nchini Uganda.
-
Utafiti: Makundi ya wanamgambo Nigeria yamepata karibu dola milioni 6 kupitia malipo ya kikomboleo
Aug 27, 2026 11:54Utafiti mpya umebaini kuwa makundi yenye silaha nchini Nigeria yamekusanya karibu dola milioni 6 kama malipo ya kikomboleo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, huku visa vya utekaji nyara vikiongezeka kwa kasi katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
-
Nigeria yaagiza kufanyika msako baada ya kutekwa nyara watu wengi
Aug 27, 2026 04:22Rais Bola Tinubu wa Nigeria ameviagiza vyombo vya usalama kuwasaka watu wenye silaha wanaotuhumiwa kuua makumi ya watu na kuwateka nyara wakazi wa vijiji vinne katika jimbo la Niger linalopatikana kaskazini- kati nchini humo.
-
WHO: Mapigano yasitishwe DRC kwa angalau miezi sita ili kukomesha mripuko wa ebola
Aug 26, 2026 11:10Wakati mripuko wa ugonjwa wa ebola unaendelea kuenea kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu kwa muda wa angalau miezi sita, ili kuwezesha timu za afya kuwafikia watu walio katika hatari na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
-
Wapinzani Sudan wapinga mazungumzo ya kitaifa ya Burhan
Aug 26, 2026 03:30Mkutano mkubwa wa makundi ya kisiasa na asasi za kiraia za Sudan zinayopinga vita umemalizika huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia.