-
Idadi ya waliokufa kutokana na hujuma ya RSF Kusini mwa Kordofan, Sudan, yafikia 114
Dec 08, 2025 23:10Mamlaka za Sudan katika jimbo la Kordofan Kusini zimethibitisha maafa makubwa: shambulio la ndege isiyo na rubani la waasi wa RSF lililotokea Alhamisi, Desemba 4, hadi sasa limeua watu 114 na kujeruhi 71. Miongoni mwa waliokufa wamo watoto 63 na idadi hiyo ingali inaongezeka.
-
Tinubu: Jeshi la Nigeria ‘lililinda’ Benin kufuatia jaribio la mapinduzi
Dec 08, 2025 23:09Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, amesema vikosi vya ulinzi vya nchi yake vilisaidia kulinda taifa jirani la Benin baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi Jumapili.
-
Ukosefu mkubwa maji unazidi kusambaa kusini mwa Somalia
Dec 08, 2025 23:08Vyanzo muhimu vya maji kusini mwa Somalia vinakauka kwa kasi huku ukame ukiongezeka, na kusababisha uhaba mkubwa kwa mamia ya maelfu ya watu.
-
Mapigano yaendelea: Makubaliano ya amani ya DRC na Rwanda yabakia kuwa ndoto
Dec 08, 2025 07:35Mapigano makali yameendelea kujiri Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakikabiliana na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na wanajeshi wa Burundi.
-
Serikali ya Tanzania yawataka wananchi wasiokuwa na dharura kubaki nyumbani Disemba 9
Dec 08, 2025 07:13Serikali ya Tanzania imewataka wananchi kusalia majumbani kesho Desemba 9, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka kama Siku ya Uhuru wa Tanganyika.
-
DRC: M23 ikisaidiwa na jeshi la Rwanda inasonga mbele kuelekea Kivu, imeteka mji wa kimkakati
Dec 08, 2025 03:01Duru za serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimetangaza kuwa, waasi wa M23, wakisaidiwa na jeshi la Rwanda wanaendelea kusonga mbele kuelekea eneo la Kivu Kusini.
-
Serikali ya Nigeria yafanikisha kuachiwa huru watoto 100 waliotekwa nyara katika jimbo la Niger
Dec 08, 2025 02:56Serikali ya Nigeria imefanikisha kuachiliwa huru watoto 100 wa skuli waliotekwa nyara mwezi uliopita katika Jimbo la Niger. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya Channels Television jana Jumapili.
-
AU, ECOWAS zalaani jaribio la mapinduzi Benin; zasema zinaiunga mkono serikali
Dec 07, 2025 23:37Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) zimelaani jaribio la mapinduzi nchini Benin siku ya Jumapili, na kueleza kuwa zinaiunga mkono serikali katika kudumisha utaratibu wa kikatiba.
-
AU yalaani shambulio la RSF lililoua zaidi ya raia 100 katika mji wa Kalogi, kusini mwa Sudan
Dec 07, 2025 23:05Umoja wa Afrika, AU umelaani vikali mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyofanywa na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, RSF yaliyoua makumi ya watu wakiwemo watoto katika mji wa Kalogi kusini mwa Sudan.
-
Mgombea urais Uganda: Nilipigwa na askari usalama
Dec 07, 2025 08:49Bob Wine au Robert Kyagulanya mgombea kiti cha urais nchini Uganda kwa tiketi ya chama cha upinzani cha NUP amesema kuwa askari usalama wa nchi hiyo wampiga yeye na wafuasi wake wakati walipokuwa katika kampeni za uchaguzi kaskazini mwa nchi hiyo katika kile kinachotajwa kuwa muendelezo wa ghasia na utumiaji mabavu unaoshuhudiwa Uganda kabla ya uchaguzi wa Rais Januari 15 mwakani.