-
Russia yaonya kuhusu kutumwa magaidi wa ISIS nchini Ukraine
Mar 06, 2022 01:19Idara ya Ujasusi wa Nje ya Russia (SVR) imesema katika taarifa yake ya siku ya Ijumaa kwamba Marekani inawapa mafunzo magaidi wa Daesh (ISIS) katika kituo cha Al-Tanf nchini Syria ili wapelekwe Ukraine.
-
Mazungumzo ya Vienna na umuhimu wa safari ya Grossi mjini Tehran
Mar 05, 2022 08:04Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ta Atomiki (IAEA) leo Jumamosi amewasili hapa Tehran na kulakiwa na Behrouz Kamalvandi Msemaji na Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Nishati ya Atomiki lal Iran. Ziara ya Grossi hapa Tehran inafanyika kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi baadhi ya hitilafu za mitazamo kuhusu faili la nyuklia la Iran pamoja na masuala mengine kati ya Iran na wakala wa IAEA.
-
Mfalme wa Bahrain atembelea Saudia mkesha wa mwaka wa 11 wa kampeni ya kijeshi
Mar 04, 2022 23:14Katika hali ambayo siku 10 zijazo itatimia miaka 10 tokea utawala wa Saudi Arabia utume wanajeshi wake Bahrain katika kampeni ya kukandamiza wananchi, mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Aal Khalifa ametembelea Saudia na kufanya mazungumzo na watawala wa Riyadh.
-
Jibu la China kwa tuhuma za Blinken
Mar 04, 2022 08:37Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin ameyataja matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken kuhusu mkoa wa Xinjiang kuwa ni shutuma zisizo na msingi. Katika ujumbe wake wa video, Blinken aliishutumu China kwa kuendeleza kile alichodai kuwa ni mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu katika mkoa wa Xinjiang.
-
Kukosoa Iran misimamo ya kindumakuwili ya madola ya Magharibi kuhusu haki za binadamu
Mar 03, 2022 22:54Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Iran ambaye pia ni mkuu wa masuala ya kimataifa katika Idara ya Mahakama ya Iran amekosoa misimamo ya kindumakuwili ya madola ya Magharibi katika suala la haki za binadamu na kusema kuwa, kadhia ya haki za binadamu haipasi kutumiwa kama wenzo wa kisiasa.
-
Sisitizo la serikali ya Taliban la kufuatiliwa mafaili ya viongozi wa zamani wa Afghanistan
Mar 03, 2022 07:49Rais wa serikali ya mpito ya Afghanistan ametoa wito wa kufuatiliwa mafaili ya viongozi wa serikali ya zamani ya nchi hiyo.
-
Kukosoa Syria na Iran vikao vya Baraza la Usalama kuhusu faili la silaha za kemikali la Damascus
Mar 02, 2022 20:29Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na faili la silaha za kemikali la Syria kilifanyika hivi karibuni na kukabiliwa na ukosoaji mkubwa wa wawakilishi wa Syria na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na utendaji wa kindumakuwili katika vikao hivyo.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; Marekani dhihirisho la “Ujahilia wa Kisasa”
Mar 02, 2022 09:26Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, uchafu mwingi wa kimaadili uliokuwa katika zama za ujahilia unashuhudiwa hii leo kwa sura pana, kubwa na ya kuratibiwa katika ulimwengu wa Magharibi unaojulikana kama uliostaarabika.
-
Vikosi vya kimataifa na kuendelea kuwepo Imarati nchini Yemen
Mar 01, 2022 22:51Kwa mara nyingine tena Imarati imeimarisha uwepo wake wa kijeshi usio wa moja kwa moja nchini Yemen kupitia mfumo wa vikosi vya kimataifa.
-
Vita vya Ukraine na mabadiliko ya uwiano wa nguvu barani Ulaya
Mar 01, 2022 06:39Kuanza vita vya Russia na Ukraine kumevuruga mlingano wa kijeshi hasa miongoni mwa mataifa ya Ulaya, kiasi kwamba Ujerumani imetenga Euro bilioni 100 kwa ajili ya bajeti yake ya kijeshi, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wake wa ulinzi.